Baraza la madiwani
halmashauri ya jiji la Arusha limemchagua Diwani wa Kata ya Kaloleni
Maxmillian Iraghe kuwa Mstahiki Meya wa jiji hilo baada ya kuwabwaga
wenzake Isaya Doita na Prosper Msofe.
Akiongea wakati
akimtangaza mshindi huyo Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha
Dkt.John Pima ambaye ndio msimamizi wa uchaguzi huo akitangaza matokeo
alisema Maxmilliani Iraghe amepata kura 29 akifuatiwa Prosper Msofe
aliyepata kura 9 huku Isaya Doita akiambulia kura 2.
Alisema kwa mamlaka
ya kisheria anamtangaza rasmi Maxmillian kuwa Mstahiki Meya wa
halmashauri hiyo ya jiji la Arusha kuongoza baraza hilo kwa kipindi cha
miaka mitano.
Mara baada ya
kutangazwa mshindi Mstahiki Meya aliwashukuru madiwani kwa kuonyesha
imani kubwa kwake na kuahidi ushirikiano na kufanyakazi kwa kasi na
weledi wa hali ya juu.
Alisema kuwa baraza
hilo chini yake litakuwa ni baraza la kuwahudumia wananchi na kuwaletea
maendeleo katika kipindi chote atakachokuwa madarakani.
Aliwaomba wananchi
kumpa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yake naye atajitahidi
kuendeleza ushirikiano na kuchapakazi usiku na mchana kuwaletea
maendeleo wananchi wa jiji la Arusha.
“Watendaji na
madiwani huu sasa ni muda wa kuchapakazi kuhakikisha ilani ya CCM
inatekelezwa kwa kiwango cha juu kila moja wetu aliahidi kuwatumikia
wananchi kwa nguvu zote tukaonyeshe hilo sasa”
Kwa Upande Mwengine
Mkurugenzi wa Jiji la Arusha alimtangaza naibu Meya wa Jiji hilo kuwa ni
Veronica hosea Diwani wa vitu maalumu kutoka kata ya Moshono
Mara baada ya
kutangazwa aliwashukuru madiwani kwa kuonyesha imani juu yake na kuahidi
kuchapakazi katika kumsaidia Mstahiki Meya kwenye majukumu ya kuongoza
baraza la madiwani ndani ya jiji la Arusha.
Alisema kuwa misingi
yake ya uongozi ni kuchapakazi na ushirikiano kwamadiwani na watendaji
ndani ya halmashauri hivyo kuhakikisha yale malipo kwenye ilani ya chama
cha mapinduzi yanatekelezwa kwa vitendo.
“Niwasihi sana tupeni ushirikiano nasi tutachapakazi kutekeleza shughuli za kuwaletea maendeleo wananchi wetu”
Post A Comment: