NA MWANDISHI WETU,ARUSHA
Jumuiya ya wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa imempongeza Rais John Magufuli na Rais wa Zanzibar Dk, Hussein Mwinyi kwa ushindi wa kishindo walioupata kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28 mwaka huu.
Pongezi hizo zimetolewa na mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Taifa Dk, Edmund Mndolwa wakati akizungumza na wajumbe wa baraza la wazazi mkoa wa Arusha sambamba na kutoa muongozo mpya wa kuendesha shule za jumuiya hiyo hapa nchini.
"Jumuiya ya wazazi wa CCM tunampongeza Rais Magufuli pamoja na Rais Mwinyi kwa ushindi walioupata ambao unatokana na utekelezaji mzuri wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015-2020 ambayo imetatua kero mbalimbali zilizokuwa zinawakabili wananchi wanyonge".
Dk, Mndolwa ametumia fursa hiyo kuwataka wenyeviti wa Jumuiya hiyo kwa mikoa yote nchini kuanzisha shule ya wasichana ya masomo ya sayansi ili kuunga mkono ilani ya CCM ya mwaka 2020-2020.
Amesema Jumuiya hiyo itaanzisha idara maalum ya ukaguzi wa shule zake kwa ajili ya kufuatilia maendeleo ya wanafunzi kitaaluma.
Amesema Jumuiya hiyo kwa sasa haina mpango wa kuunza shule zake na kwamba imepijipanga kikamilifu kwa kuwa na mwenyeviti mahiri wa bodi za shule watakaohakikisha wanaweka mazingira rafiki ya waalimu kufanya kazi ikiwa ni pamoja na kulipwa maslahi yao kwa wakati lakini pia kuboresha miundombinu ya majengo.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoa wa Arusha Hezron Mbise amesema amepokea maelekezo hayo na kwamba ofisi yake kwa kushirikiana na viongozi wa Jumuiya hiyo mkoa wa Arusha watatekeleza agizo hilo la ujenzi wa shule ya wasichana ili kuwakwamua watoto wa kike.
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya Leguruki inayomilikwa na Jumuiya hiyo Elishiliya Kaaya amesema kutokana na uzoefu wake alionao wa uenyekiti wa bodi za shule mbalimbali atautumia kuhakikisha shule hiyo inagia inafanya vizuri kitaaluma ili iingie kwenye shule 10 bora kitaifa.
"Hakuna shule mbaya, shule ili ifanye mizuri lazima waalimu wafanye kazi katika mazingira mazuri ikiwa ni pamoja na kulipwa stahiki zao kwa wakati lakini pia kutoa motisha ili kuongeza hari ya kufundisha".Naomba niwaahidi shule hii itafanya vizuri kitaaluma ndani ya muda mfupi.
Post A Comment: