Na Geofrey Stephen Arusha
JIJI la Arusha limepata Meya mpya ,Maxmilian Irange kupitia chama cha Mapinduzi na Naibu Meya wa Jiji hilo,Veronica Hosea
Akitangaza matokeo ya uchaguzi wa Meya huyo,Katibu Tawala Wilaya ya Arusha,Nyangusi Naibala alisema Irange ambaye ni meya alipata kura 32 huku kura moja ikiwa imeharibika na kufanikiwa kupata nafasi hiyo
Huku matokeo ya unaibu Meya yakiwa ni kura 33 zilipigwa ,kura halali ni 32 huku kura moja ikiwa imeharibika
Wakitoa neno la shukrani ,Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha,Joseph Massawe alisema walilima mashamba wakapalilia na kuvuna hivyo siku ya mavuno ni kushangilia
Aliwapongeza madiwani hao kwa kuchaguliwa na hawakukosea hata mmoja kichaguliwa walipimwa na kufanyiwa tathimini na kuonekana wanatosha katika kata na viti maalum
Alimpongeza Naibu Meya Veronica kwa kuchaguliwa kupata nafasi hiyo na meya pia na alitoa rai kwa madiwani kuwa chaguzi zimeisha na kama hujachaguliwa katika kamati mbalimbali au madaraka fulani usilazimishe jambo
"Tunaamini kwa Arusha ya sasa vurugu basi sababu tunadiwani mmoja kutoka Chadema huku nyie mpo 24 hivyo nawaomba mpeni ushirikioano huyu mtoto wa dawa aliyetoka upinzani"
Pia alimpongeza Mkurugenzi wa Jiji la Arusha ,John Pima kwakufanya kazi kwa bidii na kuwashukuru wananchi wa Jiji la Arusha kwa ushirikiano wanaotoa
Awali Mgombea Umeya wa Jiji la Arusha,Maxmilian Irange alisema Arusha ni Jiji la Kitalii hivyo linahitajika kuwa Jiji bora la utalii hivyo aliomba kura za ndio ili aweze kuleta aendeleo ikiwemo ukisanyaji wa mapato
Naye Mgombea Unaibu Meya wa Jiji la Arusha,Veronica akiomba kura za ndio alisisitiza kumshauri vema meya wa Jiji la Arusha pamoja na Mkurugenzi wa jiji la Arusha,John Pima
Wakati huo huo,madiwani 25 wa Jiji la Arusha pamoja na waviti maalum wamekula kiapo cha uaminifu jana kwaajili ya kuanza rasmi kwa vikao vya baraza la madiwani Jiji la Arusha
Akiongoza kiapo hicho ,Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha,Martha Mahumbuga aliwasihi madiwani hao kuheshimu viapo hivyo
Wakila kiapo baadhi ya madiwani hao,Alex Marti wa kata ya Olasiti na Abraham Mollel kata ya Kimandolu walisema kuwa wanashukuru kwa kiapo hicho sambamba na kiapo cha maadili (tamko la mali)
Awali mkurugenzi wa Jiji la Arusha ,John Pima aliwapongeza madiwani hao kwa kuapa na kusema kuwa alipokea majina ya wagombea mawili ya wagombea kwa nafasi mbili yani Meya na Naibu Meya wa Jiji la Arusha ambapo wapigakura ambao ni madiwani 33 wakiwemo madiwani viti maalum walipiga kura kwaajili ya kumchagua Meya na Naibu Meya
....
Post A Comment: