Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi akizungumza na Watendaji wa Idara ya Utamaduni na Sera na Mipango wa Wizara hiyo katika kikao cha kiutendaji kilichofanyika Novemba 24,Jijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali watu wa wizara hiyo Bw.Benard Marcelline.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi akimsikiliza Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Utamaduni wa wizara hiyo Dkt. Emmanuel Temu katika kikao cha kiutendaji kilichofanyika Novemba 24, Jijini Dodoma. Katikati ni Mkurugenzi Idara ya Utawala na Rasilimali watu wa wizara hiyo Bw.Benard Marcelline.
Na Shamimu Nyaki – WHUSM, Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi ameiagiza Idara ya Maendeleo ya Utamaduni ya Wizara hiyo kuanza maandalizi ya kuzindua Bodi ya Mfuko wa Utamaduni na Sanaa.
Katibu Mkuu Dkt.Abbasi ametoa maagizo hayo Novemba 24, Jijini Dodoma katika kikao chake na Idara hiyo.
Dkt.Abbasi ameiagiza Idara hiyo kusimamia vyema Taasisi zilizo chini yake hasa inayohusika na kukuza na kuendeleza Lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi.
Aidha, Dkt. Abbasi ameitaka Idara hiyo kuratibu matamasha mbalimbali huku akieleza nia ya kuwa na tamasha la Singeli Festival mwishoni mwa mwezi Desemba, 2020.
Post A Comment: