Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC), Elishilia Kaaya, akizungumza katika mkutano huo.
Salamu zikiendelea.
Mapokezi ya Dk.Mndolwa yakifanyika.
Mkutano ukiendelea.
Na Mwandishi Wetu, Arusha
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dk.Edmund Mndolwa amewataka wanajumuiya hiyo na wanaCCM Mkoa wa Arusha kuacha makundi na kufanya kazi baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu.
Mndolwa alitoa ombi hilo jana wakati akizungumza na wana CCM hao katika ziara yake ya kikazi ya siku moja mkoani humo.
"Hivi sasa tumekwisha maliza uchaguzi tuyaache makundi tuliyokuwa nayo tuungane pamoja tuchape kazi na kukiimalisha chama chetu" alisema Mndolwa.
Mndolwa aliwaambia wana CCM hao kuwa mwisho wa uchaguzi ndio mwanzo wa uchaguzi mwingine hivyo wasibweteke bali waanze kujipanga kwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya 2020-2025 ili waje wapate ushindi mnono kama waliopata mwaka huu.
Aidha Mndolwa akizungumza na Baraza la Wazazi la Mkoa huo alisema kila mmoja wao anapaswa kuyajua majukumu yake jambo litakalosaidia kuijenga jumuiya hiyo.
Pamoja na mambo mengine Dk. Mndolwa alitumia nafasi hiyo kufundisha masuala ya utawala bora na kukagua miradi mbalimbali inayoendeshwa na jumuiya hiyo.
Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Mkoa wa Arusha, Hezron Mbise akizungumza wakati akimkaribisha Dk. Mndolwa alimuhakikishia kuitunza na kuendeleza miradi yote ya jumuiya hiyo ukiwepo wa mashine ya kufyatulia matofari uliopo Longido mkoani humo.
Post A Comment: