KATIBU Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salimu kulia akitoa cheti kwa Maria Gaspar ambaye amenufaika kupitia mradi wao wa elimu nje ya mfumo rasmi kwa mwaka 2019 wakati wa halfa ya utoaji wa vifaa venye thamani ya Sh.milioni 29 vilivyotolewa na Shirika la BRAC Tanzania  kwa wasichana ambao walinufaika kupitia mradi wao wa elimu nje ya mfumo rasmi kwa mwaka 2019 kulia ni Meneja wa Mradi wa Elimu wa Shirika hilo Manoah William
KATIBU Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salimu kulia akitoa cheti kwa Salma Hassani  ambaye amenufaika kupitia mradi wao wa elimu nje ya mfumo rasmi kwa mwaka 2019 wakati wa halfa ya utoaji wa vifaa venye thamani ya Sh.milioni 29 vilivyotolewa na Shirika la BRAC Tanzania  kwa wasichana ambao walinufaika kupitia mradi wao wa elimu nje ya mfumo rasmi kwa mwaka 2019 kulia ni Meneja wa Mradi wa Elimu wa Shirika hilo Manoah William
KATIBU Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salimu kulia akitoa vifaa kwa Zawadi Salim  ambaye amenufaika kupitia mradi wao wa elimu nje ya mfumo rasmi kwa mwaka 2019 wakati wa halfa ya utoaji wa vifaa venye thamani ya Sh.milioni 29 vilivyotolewa na Shirika la BRAC Tanzania  kwa wasichana ambao walinufaika kupitia mradi wao wa elimu nje ya mfumo rasmi kwa mwaka 2019 wa pili kutoka kushoto ni  ni Meneja wa Mradi wa Elimu wa Shirika hilo Manoah William na
KATIBU Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salimu kulia akitoa vifaa kwa Tatu Sajala  ambaye amenufaika kupitia mradi wao wa elimu nje ya mfumo rasmi kwa mwaka 2019 wakati wa halfa ya utoaji wa vifaa venye thamani ya Sh.milioni 29 vilivyotolewa na Shirika la BRAC Tanzania  kwa wasichana ambao walinufaika kupitia mradi wao wa elimu nje ya mfumo rasmi kwa mwaka 2019 kulia ni Meneja wa Mradi wa Elimu wa Shirika hilo Manoah William
KATIBU Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salimu akizungumza wakati wa halfa hiyo
Meneja wa Mradi wa Elimu wa Shirika hilo Manoah William akizungumza wakati wa halfa hiyo
Meneja wa Mradi wa Elimu wa Shirika hilo Manoah William akizungumza
Afisa Maendeleo ya Jamii kwa Jiji la Tanga Saimoni Nende
mmoja kati ya wanufaika kwenye mradi huo akizungumza
Sehemu ya vifaa vilivyokabidhiwa
Sehemu ya vifaa vilivyokabidhiwa
Sehemu ya vifaa vilivyokabidhiwa
Sehemu ya wanufaika kupitia mradi huo wakifuatilia masuala mbalimbali

 SHIRIKA la Kimataifa la Maendeleo ya Vijana BRAC Tanzania limetoa msaada wa vifaa venye thamani ya Sh.milioni 29 kwa wasichana ambao walinufaika kupitia mradi wao wa elimu nje ya mfumo rasmi kwa mwaka 2019.


Akizungumza wakati wa halfa ya utoaji wa vifaa hivyo, Meneja wa Mradi wa Elimu wa Shirika hilo Manoah William alisema wasichana hao ni wale ambao hawakuweza kufanikiwa kufanya vizuri kwenye mitihani yao katika mpango huo ambao walikuwa wakiutekeleza kwa kushirikiana na serikali.

Alisema mpango huo ulianza mwezi Septemba mwaka huu kwa kushirikiana na serikali kupitia Shirika la viwanda vidogo vidogo (Sido) ambao mabinti zaidi ya 120 walipelekwa kwenye mafunzo na kujifunza ujasiriamali na stadi mbalimbali.

Manoah alisema katika mafunzo hayo yalijifunza aina mbili ya usindikaji wa chakula na kutengeneza sabuni ambao wanaamini itakuwa mkombozi kwao kuweza kujikwamua kiuchumi wao na jamii zao.

“Licha ya kutokufanikiwa lakini bado walitakiwa kuendelea na elimu shirika likaona hapana kwa sababu hawakufanikiwa hai maanishi kwamba watashindwa kuendelela kimaisha kwa hiyo tukawa na mpago wa kuwasaidia na kuweza kupata mafunzo haya”Alisema

“Tunaamini mafunzo walioyapata wataweza kujiajiri wenyewe tunawashukuru sido baada ya kupokea vyeti wanafunzi hao wataendea kupata sapoti kwa sido moja kwa moja ikitokea washiriki maonyesho, mashindano mbalimbali na Sido watakuwa sambamba nao”Alisema

Hata hivyo alisema pia mradi huo utafanikiwa zaidi ili kuweza kuwaunganisha na Shirika la Viwango nchini (TBS) ili bidhaa zao ziweze kutambulika na kuwa wafanyabishara wao wanajisikia fahari.

“licha ya watu kushindwa kuendelea na shule lakini wamefanikiwa kujiajiri na kuajiri baada ya hapa mpango wetu ni kuendelea kuwafuatilia kuona wanaendele na kazi zao kwa kushirikiana na serikali za kata,mitaa na wilaya ili kuona wanaendeleaje”Alisema

Awali akizungumza katika halfa hiyo Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salim alisema alilishukuru Shirika la BRAC Tanzania kwa kuisaidia serikali katika kuhakikisha wasichana walio nje ya mfumo rasmi wanapata elimu ili kutimiza ndoto zao.

Alisema kwani wanapokuwa wakiwasaidia mabinti hao wanakuwa wameisaidia jamii nzima hivyo niwapoingez sana kwa kusaidia serikali kuongeza vipato vya wananchi.

“Wapo wasichana wengi sana mtaani lakini nyie leo mmebahatika kufika hapa nawasihi mkatumie vema vifaa mlivyopewa kuweza kujikwamua kiuchumi na sio vyenginevyo “Alisema

Aliwaasa pia kuhakikisha vifaa hivyo wanavitumia kwa malengo yaliyokusudiwa ili viweze kuwa chachu yao kuweza kujikwamua kiuchumi wao na jamii zinazowazunguka

“Lakini pia nawaasa mafunzo mliyopewa mkayafanyie kazi na tafuteni wateja pia jitahaidini kutafuta masoko na kutengeneza ubora wa bidhaa zenu ambazo mtakuwa mkizalisha”Alisema

Naye kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii kwa Jiji la Tanga Saimoni Nende alisema kwamba kazi iliyofanywa na Shirika la BRAC Tanzania nzuri na inapaswa kupongezwa.

“Kwa kweli nimefurahishwa na Shirika la BRAC kazi kubwa mnayofanya ya kuwaendesha wasichana walio nje ya mfumo rasmi wa masomo najua wengi hawakupenda kukutana nah alai hii lakini mlipata tatizo kutokana na mazingira yaliyokuwepo”Alisema

Hata hivyo alitoa wito kwa wasichana hao kwamba walichokipata wakakitumuia vizuri kiweze kuwasaidia huku akieleza kwa waliopata ujuzi huo katika kata mbalimbali wao wataendelea kuwafuatilia na kuwa karibu nao.

Mwisho.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: