|
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa kushoto akimkabidhi msaada wa taulo za kike Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(RAS) Judica Omari katika kwa ajili ya wasichana kwenye shule ya Sekondari Old Tanga zenye thamani ya Milioni 5,kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Old Tanga Kasimu Ndumbo wa kwanza kulia ni Afisa Elimu Mkoa wa Tanga Mayansa Hashimu na wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) Faidha Salim
|
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa kushoto
akimkabidhi msaada wa taulo za kike Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(RAS)
Judica Omari katika kwa ajili ya wasichana kwenye shule ya Sekondari Old
Tanga zenye thamani ya Milioni 5,kulia ni Mwalimu Mkuu wa shule ya
Sekondari Old Tanga Kasimu Ndumbo wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya
ya Tanga (DAS) Faidha Salim
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa akizungumza wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano
KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari akizungumza wakati wa halfa hiyo
AFISA Elimu Mkoa wa Tanga Mayansa Hashimu akizungumza wakati wa halfa hiyo
Meza kuu wakiwa wamesimama wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kupokea msaada huo
Sehemu ya walimu na wanafunzi wa shule ya Sekondari Old Tanga wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye halfa hiyo
Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Old Tanga akitumbuiza kwenye halfa ya makabidhiano hayo
|
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Old Tanga wakiiimba wimbo wa Taifa kabla ya kupokea msaada huo
BENKI ya CRDB imetoa msaada wa taulo za kike zenye thamani
ya sh.milioni 5 katika shule ya Sekondari Old Tanga ya Jijini Tanga ili
kuwasaidia watoto wa kike kusoma kwenye mazingira salama hali
itakayowasaidia kuongeza bidii kwenye masomo yao.
Akizungumza
wakati wa hafla ya makabidhiano hayo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga
Judica Omari, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini Chiku Issa
alisema kwamba wametoa msaada huo kupitia kampeni maalumu ya Hedhi
Salama kwa elimu bora.
Alisema kwamba Benki ya CRDB inachukua
kwa uzito sana suala la uwezeshwaji mtoto wa kike,mwanamke hatua ambayo
imepelekea benki yao kutunga na kutekeleza sera na mikakati inayolenga
kuhamaisha usawa wa kijinsia na kutengeneza mazingira rafiki kwa
mwanamke.
Meneja huyo alisema kwamba ndani ya benki yao
wamefanya hivyo wakiamini kuwa ukimuewezesha mwananke umeiwezesha jamii
na hivyo ndio moja ya siri kubwa ya mafanikio kwenye benki hiyo.
Alisema
benki hiyo waliamua kuanzisha mpango huo lakini kwa bahati kubwa shule
ya Sekondari Old Tanga wakawa ni miongoni mwa shule ambazo wanaanza
nazo.
“Pamoja na jitihada zinazofanywa na wadau mbalimbali
ikiwemo serikali bado mahudhuria ya watoto wa kike mashuleni
hayaridhishi na hivyo kupelekea kutokufanya vizuri katika masomo yao
“Alisema
Alisema changamoto hiyo kwa kiasi kubwa imechangia
watoto wengi wa kike wakati wanapoingia kwenye kipindi chao cha hedhi
kutokuwa na uwezo wa kuwa na taulo bora za kike inawalazimu kukaa
nyumbani na kushindwa kwenda shule na kukaa nyumbani mpaka
watakapomaliza .
Meneja huyo alisema lakini au kuvaa vitambaa
ambavyo sio salama kwa afya zao ambapo alieleza kwamba utafiti
uliofanywa na Taasisi ya Taifa ya Magonjwa ya Binadamu NIMR unaonyesha
kuwa katika wilaya 14 za Tanzania Bara ulibaini kuwa asilimia 15 ya
wanafunzi wa kike wanashindwa kuhudhuria shule katika siku zao za hedhi.
Alisema katika ya hizo asilimia 42 inachangiwa na ukosefu wa
vifaa vya hedhi na 34 asilimia hofu ya kujichafua kwa sababu hana kitu
sahihi cha kujistiri huku asilimia 26 inatokana na miundombinu isiyokuwa
rafiki wakati akiwa kwenye kipindi cha siku zake.
“Kutokana na
changamoto hiyo benki ya CRDB tuliamua kuanzisha kampeni maalumu
ijulikanayo Hedhi Salama kwa elimu bora inayolenga kutatua changamoto
wanazopata watoto wa kike kwa kutoa msaada wa taulo za kike kwenye shule
mbalimbali nchi nzima”Alisema
Aliongeza kwamba wao kama benki
wanaamini upatikanaji wa taulo za kike ni muhimu kwa mahudhurio ya mtoto
wa kike shuleni na kupata haki yake ya msingi wa elimu sawa na mtoto wa
kiume
Awali akizungumza wakati wa makabidhiano hayo Katibu
Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari aliwashukuru Benki ya CRDB kutoa
msaada huo ambao utasaidia katika kuboresha masomo yao.
“Kwa
kweli niwashukuru sana na kuwapongeza uongozi wa Benki ya RCD kwa
kutambua umuhimu wa huduma hii kwa mtoto wa kike kwenye mkoa wa Tanga
nimefurahihwa sana kwa kujali na kutoa mahitaji haya ambayo ni muhimu
kwa vijana wetu wa kike”Alisema Ras Judica.
Aidha alisema kwamba
serikali ya awamu ya tano nchini ya Rais Dkt John Magufuli inatoa
kipaumbele kwenye kuboresha elimu na shule nyingi zimepewa kipaumbele
cha hali ya juu.
Alisema katikampango wa elimu ya bila malipo
imeongeza zaidi idadi ya wanafunzi kuanzia darasa la kwanza hadi kidato
cha kwanza na ufadhili huo ambao umepatikana ni mkubwa kutokana kwa
serikali ya awamu ya tano huku akieleza kwamba kwa mkoa wa Tanga
umeendelea kupokea msaada huo.
Katibu Tawala huyo alisema kila
mwezi kwa mkoa wa Tanga wanapokea kiasi cha sh.Bilioni 1 kwa ajili ya
kuendesha mpango wa elimu bure katika shule na mpango huo unasaidia
katika kutoa posho mbalimbali kwa ajili ya uwezeshwaji wa wanafunzi,
wakuu wa shule wanawezeshwa
Alitaja pia uwezeshwaji wa walimu
wakuu pamoja na maafisa elimu kata ambao ni viongozi muhimu katika
kuhakikisha elimu bora inapatikana mkoani
“Katika ngazi ya shule
fedha hizo pia zinatumika kwenye masuala ya kujenga taaluma, kufanya
ukarabati, utawala, kununua vifaa, usimamizi mitihani katika hiyo fedha
pa asilimia 10 inatumika kwenye kununua mahitaji mbalimbali kwa ajili ya
kumuwezesha mtoto wa kike kuweza kufanya ufaulu mzurina kuweza kukaa
shuleni kwa utulivu”Alisema |
|
|
|
Post A Comment: