NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.


Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Arusha mjini Dr John Pima amewaapisha mawakala elfu 11,311 wa vyama vya siasa kati ya elfu huku 522 wakitakiwa kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza katika barua zao.


Akiongea na waandishi wa habari Dr Pima alisema kuwa alipokea  barua elfu 11,833 kutoka vyama 15 vya siasa ambavyo ni CUF, CHADEMA ,CCK, CCM, ACT, UDP, DEMOKRASIA MAKINI, ADA TADEA, CHAMA CHA SAUTI YA UMMA, UMDP, NRA,AAFP, ADC, UPDP pamoja na NCCR MAGEUZI.


Alieleza kuwa baada ya kuzipokeabarua hizo na kuzikagua yalibainika mapungufu mbalimbali ambayo ni kutoonyesha majina ya kata na vituo watakavyosimamia, barua kutosainiwa na katibu wa chama aliyewatambulisha, nakala za vitambulisho kutoonyesha taarifa zozote za wakala, kutumika kwa mihuri tofauti katika barua zilizotoka chama kimoja ikiwa ni pamoja na mawakala kutambulishwa na katibuwa jimbo badala ya katibu wa wilaya .


“Pia kulikuwa na changamoto nyingine ndogondogo  ambapo leo asubuhi tumeita vyama vyote na kuwaeleza mapungufu hayo navingi vimeshafanya marekebisho huku tukiwapa wengine muda wa marekebisho kufikia mchana wa leo kwajili ya kukidhi vigezo na kuabishwa pamoja na kuruhusiwa kuendelea na hatua nyingine” Alisema Dr Pima.


Alifafanua kuwa kwa mujibu wa ratiba ya tume ya taifa ya uchaguzi ratiba iliyopo jimbo la Arusha mjini ni kuteua na kuapisha mawakala kutoka vyama vyote15 vitakavyoshiriki uchaguzi mkuu october 28 mwaka huu.


Aidha  alitoa wito kwa mawakala  wote kuzingatia maelekezo yaliyotolewana tume ya taifa ya uchaguzi kama sheria, kanuni, miiko, maadili na taratibu za kuzifuata zoezi zima la usimamizi wa uchaguzi lakini pia wito kwa wananchi wa jimbo la Arusha mjini kuwa watulivu na tayari kwa zoezi la upigaji kura.


“Niwahakikishie kuwa maandalizi ya uchaguzi yanaenda vizuri, na tayarikwa kumfanya mwananchi wa Arusha kupiga kura kwa utulivu na amani siku ya jumatano october 28 katika kituo chake alichojiandikishia” Alisema

Share To:

msumbanews

Post A Comment: