Mhandisi
Karoli Lihala akijibu swali kutoka kwa katibu wa Skimu ya umwagiliaji
Isenyela Bw. Samweli Ngeve wakati wa Mafunzo Chimala Wilayani Mbarali
Leo.
Baadhi ya Wakulima katika picha wakisikiliza mada
Na Mwandishi Wetu, Chimala Mbarali
Wakulima katika Skimu ya Isenyela wamepewa mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika kilimo cha umwagiliaji katika siku nyingine ya mafunzo kwa wakulima hao.
Akitoa moja ya mada mhandisi Karoli Lihala kutoka Wilayani Mbarali
amewaeleza wakulima hao kuwa,ujenzi wa tuta katika njia ya kupeleka maji
mashambani ni njia nzuri ya kuimairisha sehemu ya juu ya mto.
Alisema kuwa, kusakafiwa kwa mifereji na kujengwa kwa makaravati kunaweza kuimarisha zaidi skimu hizo.
Aliongeza kwa kusema kuwa kabla ya miundombinu ya umwagiliaji
kuboreshwa na serikali “kwa sasa wakulima anaweza kuzingatia utunzaji wa
mazingira kwa kutoa mchanga katika mto, kulinda vyanzo vya maji, kutoa
magugu maji na kutofanya shughuli za kibinadamu kama kilimo katika
vyanzo vya maji.” Alisisitiza
Post A Comment: