Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Agri Thamani Foundation,Neema Lugangira na Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini wa Kituo cha Utafiti wa mbogamboga na matunda cha Kimataifa cha World Vegetable Center,Dk.Gabriel Rugalema wakiwa kwenye picha ya pamoja huku wakionyesha mkataba huo baada ya kuusaini.
Na MWANDISHI WETU-ARUSHA
MKURUGENZI wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Agri Thamani Foundation,Neema Lugangira ,leo (Oktoba 5,2020),amesaini mkataba wa makubaliano kati ya shirika hilo na Kituo cha Utafiti wa mbogamboga na matunda cha Kimataifa cha World Vegetable Center,utakaosaidia kuboresha lishe.
Shirika la Agri Thamani lililojikita kwenye kuchangia kutokomeza udumavu na utapiamlo lenye makao yake makuu mkoani Kagera,linafanya kazi ya kutoa elimu ya lishe kwenye shule,kaya na jamii na kuhamasisha kilimo lishe.
Mkataba huo wa makubaliano umesainiwa jijini Arusha ambapo makubaliano hayo yapo kwenye maeneo saba ikiwemo kuhamasisha ulaji wa mbogamboga na matunda kama sehemu ya kuimarisha lishe bora na kuwezesha kutokomeza udumavu na utapiamlo.
Akizungumza wakati wa tukio hilo,Neema ambaye pia ni Mbunge Mteule wa Viti Maalum(CCM),Kundi la Asasi za Kiraia (NGO’s),Tanzania Bara,alisema katika mkataba huo wa miaka mitano wanatarajia kuanza kuutekeleza katika mikoa saba hapa nchini.
Alitaja mikoa hiyo ni Kagera,Tanga,Kigoma,Dodoma,
Alisema kuwa wanatarajia kuanza zoezi hilo la kuanzisha bustani hizo mwezi huu katika Manispaa ya Bukoba,ambapo baada ya kumaliza katika halmashauri hiyo wataanzisha bustani hizo katika shule zingine za mikoa hiyo saba.
“Tutaanzisha bustani za mboga lishe za mfano kwenye shule zote,watoto chini ya umri wa miaka mitano,wazee na wenye uhitaji mkubwa wa lishe.Na tumeamua kuchagua mikoa hii kwa sababu inaongoza kwa changamoto ya ulaji wa mboga na matunda uko chini,”alisema
Awali Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini wa kituo hicho,Dk.Gabriel Rugalema,alitaja maeneo mengine waliyoingia makubaliano ni pamoja na kueneza elimu ya kilimo na lishe kwa jamii,kuweka msukumo katika ulaji wa mboga na matunda,kusaidia kuanzisha bustani za mboga na matunda shuleni.
Nyingine ni kusaidia kutunga sera na mipango kazi ya Taifa rafiki kwa tasnia ya kilimo cha mbogamboga na lishe,kuwafikia na kuhamasisha waandishi wa habari kama wadau maalum wa kusaidia na kueneza elimu ya lishe na kuangazia akina mama na vijana katika uzalishaji wa mazao ya mbogamboga.
Aidha Kituo hicho kilitoa pakiti 500 za mbegu za mbegu bora za mgoga mchanganyiko zenye viini lishe ambazo ndizo zitaanza kwenda kutumika kwa ajilli ya bustani hizo za mfano katika mikoa hiyo ambayo inaanza kutekeleza makubaliano hayo.
“Tutashirikiana kutafuta wadau wengine ambao tutashirikiana nao ili tuweze kufanikisha hili kwani tumeona ni la muhimu ndiyo maana tumekubali kushirikiana nao,tunaamini ukipeleka elimu hii kwa wakulima wa kawaida utajenga uwezo wao wa lishe na kiuchumi kwani Tanzania ina chakula lakini haina lishe bora,”alisema Dk. huyo
Post A Comment: