Mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Teresia Mtewele akiongea na wanawake wa tarafa ya Pawaga wakati wakiweka mikakati ya kupata kura nyingi za wagombea wa CCM wote
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Iringa Nocolina Lulandala akisisitiza jambo wakati wa kuomba kuwaomba wanawake wa UWT tarafa ya Pawaga kwa ajili ya kuzitafuta kura za wagombea wa chama cha mapinduzi
Na Fredy Mgunda,Pawaga.
UMOJA wa wanawake Mkoa wa Iringa
(UWT) wameeendelea kuzitafuta kura za chama cha mapinduzi (CCM) kata kwa kata
kwa lengo la kuhakikisha wanapata kura nyingi za mgombea urais wa chama cha mapinduzi (CCM) Dr John
Pombe Magufuli,madiwani na wabunge ili chama hicho kiendelee kushika dola.
Akizungumza kwenye
mkutano wa wananwake wa tarafa ya Pawaga mwenyekiti wa UWT mkoa wa Iringa
Nicolina Lulandala aliwaomba wanawake wote wa tafara hiyo kuhakikisha
wanazitafuta kura nyingi za wagombea wa chama cha mapinduzi ili wawee kushinda
kwa kishindo.
Alisema kuwa
Rais Dr Magufuli amefanikiwa kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa elimu
bure,kukarabati majengo ya shule na kujenga majengo mapya mengi na amefuta
michango shuleni hivyo wanawake wa Iringa wanapaswa kumtafutia kura Dr John
pombe Magufuli.
Lulandala aliongezea
kwa kusema kuwa katika sekta ya elimu wanafunzi wa vyuo vikuu wamekuwa wanapana
mikopo kwa wakati na ndio maana kwa kipindi cha miaka mitano hakuna maandamano
ya wanafunzi wa vyuo vikuu kama ilivyokuwa miaka ya huko nyuma.
Lulandala aliwaomba
wanawake wa mkoa wa Iringa kutumia ushawishi wao kuhakikisha wanampigia kura
nyingi mgombea huyo wa chama cha mapinduzi Dr John pombe Magufuli kwa kuwa
anauwezo wa kuliongoza taifa hili kimaendeleo kuliko wagombea wengine.
Alisema kuwa umoja wa wanawake Mkoa wa Iringa
(UWT) unafanya ziara
katika tarafa zote mkoa wa Iringa ili kuhakikisha wanawake wa mkoa wa Iringa wanakwenda
kuzitafuta kura za chama cha mapinduzi (CCM) kuanzia udiwani,ubunge hadi urais
hivyo wanawake waliohudhulia kongamano hilo lilikuwa na lengo la kuhakikisha
CCM inapata kura za kutosha kuliko vyama vingine.
Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT mkoa wa Iringa
Nocolina Lulandalai alisema kuwa
chama cha mapinduzi Iringa vijijini kimejipanga kuhakikisha kinaleta maendeleo
katika kata ya tarafa ya Pawaga kwa kuwa tayari wamejipanga kwa mikakati imara
ya kufanya kazi za kimaendeleo.
“Najua kina
mama wanajua kukiwa na tatizo kiafya hakuna shughuli za kimaendeleo ambazo
zitafanyika kwa urahisi hivyo tupeni miaka mitano hii tuboreshe sekta ya afya
kwa kuwa viongozi wa CCM wamejipanga kutatua tatizo hilo kama ambavyo tayari
tumejenga hospitali ya wilaya hapa Pawaga na tunaendelea kuboresha vituo vya
afya”alisema Hongoli
Aidha Hongoli alisema kuwa
tatizo la maji kwenye baadhi ya vijiji na vijiji vingine tatizo hilo
limetatuliwa kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya awamu ya tano
chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufulu kwa
ushirikiano na mbunge wa jimbo la Isimani William Lukuvi.
Alisema kuwa wananchi wa tarafa ya Pawaga wanategemea
kilimo kwa kiasi kikubwa hivyo ni lazima kuwasaidia kupandisha thamani ya mazao
ili wakulima hao wapate faida ya kilimo hicho.
Naye Mjumbe wa
halmashauri kuu ya taifa ya chama cha mapinduzi (CCM) MNEC Teresia Mtewele
ambaye alikuwa mgeni aliwaomba wanawake wa tarafa ya Pawaga kuhakikisha
wanazitafuta kura za wagombea wanaotokana na chama cha mapinduzi (CCM) ili
kuhakikisha maendeleo ya Tarafa hiyo.
Akizungumza
kwenye mkutano wa mkutano wa wanawake wa Tarafa ya Pawaga, Mtewele alisema kuwa
wananchi wanapaswa kuwachagua wagombea wa chama cha mapinduzi kwa kuwa chama
hicho ndio kinaweza kuleta maendeleo tofauti na vyama vingine
Alisema kuwa
chama cha mapinduzi kimejipanga kuhakikisha kinaleta maendeleo katika tarafa ya
Pawaga kwa kuwa tayari wamejipanga kwa mikakati imara ya kufanya kazi za
kimaendeleo.
Aidha Mtewele
alisema kuwa tatizo la maji limetatuliwa katika kata hizo kutokana kazi kubwa
iliyofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dr John Pombe Magufulu.
Alisema kuwa
wananchi tarafa ya Pawaga wanategemea kilimo kwa kiasi kubwa hivyo ni lazima
kuwasaidia kupandisha thamani ya mazao ili wakulima hao wapate faida ya kilimo
hicho.
Mtewele
alimazia kwa kuwaomba wanawake wa Pawaga kumchagua mgombea udiwani,ubunge na
mgombea urais wa CCM kwa kuwa hao ndio wanaweza kuleta maendeleo ya kweli kwa
wananchi wa kata hizo.
.
Post A Comment: