BALOZI wa China Wang Ke akiwa anasisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Agri Thamani Foundation Neema Lugangira
BALOZI China Wang Ke na Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Agri Thamani Foundation Neema Lugangira wakikabidhiana makubaliano ya ushirikiano waliyoyasaini leo Octoba 14,2020
BALOZI wa China Wang Ke na Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Agri Thamani Foundation Neema Lugangira wakionyesha makubaliano ya ushirikiano baina ya Ubalozi wa China na Agri Thamani Foundation
 

UBALOZI wa China umeingia Makubaliano ya Kushirikiana na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Agri Thamani Foundation katika maeneo ya afya, elimu na kilimo kwa wanawake na mabinti hapa nchini.

Akizungumza wakati wa utiliaji saini makubaliano hayo yaliyofanyika Ubalozi wa Chini Jijini Dar es Saaalm Balozi wa chini nchini Wang Ke alisema ubalozi huo upo tayari kuchangia maendeleo ya jamii kwa wanawake na mabinti kutoka mikoani/vijijini na imekuwa ikitoa misaada mbalimbali  

Alisema kwamba Octoba 11 mwaka huu ilikuwa ni Siku ya Watoto wa Kike Duniani hivyo katika kuenzi siku hiyo katika makubaliano yaliyosainiwa leo Ubalozi huo umetoa msaada kwa Agri Thamani wa kununua taulo za kike kwa ajili wanafunzi wa sekondari wa kike 1,500.

Balozi huyo alisema taulo hizo za kike zitapelekwa kwenye Mikoa ya Kagera, Geita, Kigoma, Tabora, Tanga, Dodoma na Lindi ambapo watoto hao wa kike watatoka kwenye familia zenye uhitaji mkubwa zaidi na watapata msaada huu kwa kipindi cha mwaka mzima ili masomo yao yasiathirike. 

Aidha pia balozi alisema mkataba huu umesainiwa leo siku ya Nyerere ikiwa pia ni sehemu ya kumuenzi maana aliwahi kusema Tanzania itapambana na adui wakubwa watatu katika maeneo ya elimu, umaskini na afya .

“Mkataba huu ambao Ubalozi wa China na Agri Thamani imesaini leo tarehe 14/10/2020 ni jitihada za kuendelea kuenzi maneno ya Nyerere na kuyaishi kwa vitendo lakini pia kudhihirisha ushirikiano mkubwa baina ya China na Tanzania”Alisema Balozi huyo.

Awali akizungumza wakati wa makubaliano hayo Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Agri Thamani Foundation Neema Lugangira  alianza kumshukuru Balozi Wang Ke kwa utayari wake wa kushirikiana na Agri Thamani huku akieleza huo ndio utakuwa mwanzo na wamejipanga kushirikiana katika maeneo mahsusi yatakayopelekea kumuinua mwanamke kiuchumi kwani ukimwezesha mwanamke na mtoto wa kike utakuwa umeiwezesha jamii nzima.

Aidha alisema Shirika hilo la Agri Thamani linatoa elimu ya Lishe kwenye Shule za Sekondari na Masuala ya Hedhi Salama na Afya ya Binti ikiwa ni sehemu ya Lishe Bora hivyo anaamini kuwa msaada huu wa taulo za kike kwa wanafunzi wa sekondari 1,500 utakuwa msaada mkubwa sana kwa mabinti hawa hususan kwa wale ambao watakuwa kwenye mwaka wa mitihani ikiwemo Kidato cha 2 na cha 4 ambao ndio walengwa. 

Hata hivyo alisema kwamba ni matarajio yao kuwa mpango huo utakuwa endelevu ili iweze kufikia wanafunzi wa kike wengi zaidi kwa kutumia ubunifu na teknolojia mbalimbali kuhakikisha wanaondokana na changamoto ya kukosekana kwake.


Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: