Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kupitia muonekano mpya linataraji kujenga vituo mia moja kwa kushirikiana na halmashauri tofauti na sekta binafsi hapa nchini.

 Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Meneja Mawasiliano na Mahusiano wa TPDC Bi. Marie Msellemu wakati akielezea harakati zao za kubadilisha muonekano wa TPDC Uliodumu kwa miaka hamsini yenye mafanikio.

 Msellemu amesema shirika hilo la maendeleo ya Petroli nchini kwa miaka hiyo hamsini limefanikiwa kuwa na kampuni tanzu mbili Gaspo na tanoil na kupitia sheria mpya ya mwaka 2015 shirika limekuwa na majukumu mapya ambayo yameifanya tpdc kujiendesha kibishara. 

 Akifafanua namna ya upatikanaji wa muonekano huo mpya kwa kubadilisha nembo Msellemu amesema watatumia wabunifu wa ndani kupata nembo hiyo mpya kupitia ushindani. 

  Baada ya sheria ya mafuta ya mwaka 2015 TPDC imeondolewa hadhi ya udhibiti na kuwa shirika la biashara kwa kutafuta ,kuendeleza na kusambaza gesi asilia pamoja na bidhaa zake.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: