Katibu Mtendaji TCU, Prof.Charles Kihampa akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi ya Tume hiyo Jijini Dar es Salaam. |
Katibu Mtendaji TCU, Prof.Charles Kihampa akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi ya Tume hiyo Jijini Dar es Salaam.
Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imetangaza awamu ya pili ya udahili wa shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2020/2021 ambapo utaanza rasmi Oktoba 12 hadi 18 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji TCU, Prof.Charles Kihampa amesema kuwa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombin ya udahili au hawakudailiwa katika awamu ya kwanza kutokana na sababu mbalimbali watumie fursa hiyo kwa kutuma maombi yao kwenye vyuo wanavyovipenda.
Aidha Prof.Kihampa amesema kuwa tume inaelekeza Taasisiya Elimu ya Juukutangaza programu ambazo bado zina nafasi.
"Waombaji na vyuo wanahimizwa kuzingatia utaratibu wa udahili kwa awamu ya pili kama ilivyooneshwa kwenyen kalenda ya udahili iliyotolewa na TCU kama inavyooneshwa kwenye tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz)". Amesema Prof.Kihampa.
Pamoja na hayo Prof.Kihampa amesema kuwa jumla ya Waombaji 90,572 wametuma maombi ya kujiunga katika vyuo 74 vilivyoidhinishwa kudahiliwa katika awamu ya kwanza ya udahili wa mwaka wa masomo 2020/2021.
Hata hivyo amesema kuwa waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja wanahimizwa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia Oktoba 9 hadi 17 mwaka huu kwa kutumia ujumbe mfupi wenye namba maalum ya siri uliotumwa kupitia namba zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili.
Post A Comment: