Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Rehema Nchimbi (kushoto) akimkabidhi juzi Mwalimu Mstaafu kutoka Wilaya ya Singida Amosi Njoghomi kiasi cha shilingi milioni 18.8 zilizookolewa kutoka kwa mmoja wa wakopeshaji wa ‘Riba Umiza.’ Mwalimu Njoghomi alikopa shilingi milioni 2, lakini mkopeshaji alimtaka arejeshe fedha taslimu shilingi milioni 31 hadi serikali ilipoingilia kati na kumsaidia.
Na Edina Alex, Singida
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Singida imeokoa sh.milioni 33.5 walizokopeshwa watumishi wa umma wastaafu na makampuni ya kukopesha fedha zenye riba kubwa maarufu kama mikopo umiza bila ya kufuata sheria.
Akitoa taarifa ya utekelezaji huo juzi Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Singida, Adili Elinipenda alisema operesheni hiyo wameifanya kufuatia agizo la mkuu wa mkoa huo la kuwatokomeza wakopeshaji haramu ambao wamekuwa wanawakandamiza wananchi hasa watumishi wa umma wanao karibia kustaafu.
"Mheshimiwa mkuu wa mkoa Takukuru mkoani hapa tumejipanga kikamilifu kuhakikisha hawa wakopeshaji umiza tunawamaliza kabisa ndani ya mkoa wa Singida na kwa kukuhakikishia leo utawakabidhi wahanga kiasi cha sh. mil 33.5 zilizotoka kwa wakopeshaji haramu. "alisema Elinipenda.
Aidha Elinipenda aliyataja makampuni hayo yaliyorudisha fedha za wananchi na watumishi wa umma kuwa ni kampuni ya Bomang Microfinance ya Singida mjini ambayo ilimkopesha Mwalimu Mstaafu Albert Sungi Mpashi kiasi Cha shilingi 7,200,000 na kumtaka arejeshe shilingi 17,000,000 huku million 18,800,000 zimeokolewa kutoka kwa mkopeshaji Biseko Mungeta Kazungu wa Singida mjini nae alimkopesha Mwalimu Mstaafu kiasi Cha shilingi Mlion 2,000,000 na kumtaka arejeshe shilingi Milioni 31,000,000.
Wengini ni kampuni ya Magirei Company Lmt (Micro Credit) ya Singida mjini imerejesha fedha za Garase Kajuna shilingi 17,000,000 , Huku Widop Company Ltd.
ikirejesha shilingi 2400,000 kwa bi Lucia Petro Nyika Muuguzi Mstaafu huku wengine ni Angelva Financial Lmt na Mwita Creditors ya Manyoni.
Kwa upande wao wahanga hao Albert Sungi , Garase Kajuna na bi Lucia Nyika walimshukuru Raisi Mgufuli na uongozi wa Serikali ya awamu ya tano kwa kuwakumbuka wanyonge maana baadhi yao walisha poteza matumaini ya kuishi kama watumishi wastaafu'
"Tunamshukuru Rais wetu Magufuli hakika Mungu ametuletea nabii sio tu Rais kwani kwetu amekuwa baba wa wanyonge tulipoteza matumaini kabisa lakini kwa uongozi wake makini tunacheka na kutabasamu" alisema mmoja wa wahanga hao.
Aidha wamewashauri watumishi wengine ambao bado wapo katika utumishi kujiandaa vuzuri ili wanapo achana na utumishi wasijiingize kwenye mikopo hiyo maana wakopeshaji hao haramu au umiza wanawatamani wastaafu au waliokwisha kustaafu.
Akikabidhi fedha hizo kwa wahanga hao Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk. Rehema Nchimbi aliwapa pole na kuwahakikishia kuwa wakopeshaji haramu ndani ya mkoa huo lazima wabadilike na kufanya kazi zingine huku akiwapongeza watumishi wa TAKUKURU kwa utekelezaji kazi hiyo.
"Mbadilike nyie wakopeshaji umiza hivi hamuogopi Mungu alichokopa mtu na anachorejesha mbona haviringani lazima tuwatokomeze hii sio Serikali ya mchezo mchezo ." alisema Nchimbi.
Post A Comment: