NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA


Wanachama wa vyama vya ushirika(Saccos) wametakiwa kujifunza namna ya kutumia teknolojia za kifedha pamoja kuwekeza katika mifumo hiyo kwani teknolojia haikwepeki.

Rai hiyo ilitolewa na makamu mkuu wa chuo cha Ushirika Profesa Alfred Sife wakati akifungua maadhimisho ya siku ya vyama vya ushirika ambapo alisema kuwa teknolojia inakua kwa kasi na vyama ambavyo ni taasisi za kifedha wanapaswa kuingia katika teknolojia ili kurahisisha upatikanaji wa huduma.

“Teknolojia itatuwezesha mtu anapotaka mkopo aweze kuomba na kupata kwa haraka  lakini pia chukueni tahadhari ili mifumo mtakayokuwa nayo isiingiliwe na waalifu, Alisema Profesa Sife.

Alieleza kuwa kama taasisi zingine za kibenki zinavyotumia mifumo ya kiteknoloji na saccos pia mnaweza kutumia hivyo jifunzeni namna ya kutumia lakini pia mkumbuke kuchukua taadhari dhidi ya waalifu.

Paulo Maiko Nandia Mkurugenzi mtendaji wa mifumo wa kifedha wa kutunza na kutoa taarifa za wanachama wa vyama vya ushirika (Tanzania Mentors Action) alieleza kuwa tumeona tutumie mfumo wa teknolojia ili kuondoa changamoto zilizokuwepo awali za wanachama kusumbuka kutoa na kufuata taarifa zao umbali mrefu.

“Mfumo huu ni suluhisho kwa Saccos kwani kuna changamoto kubwa ya wanachama kulazumika kusafiri hivyo endapo mfumo huu  hawatalazimika kwenda kutoa taarifa zao kwa kusafiri umbali mrefu bali popote waliopo wataweza kupata na kutoa taarifa zao” Alieleza Paulo

Alifafanua kuwa katika ngazi ya wanachama watatumia simu zao za mkononu kuomba mkopo, kupata na kufanya marejesho na katika ngazi ya saccos yenyewe watakuwa na taarifa zilizokwisha andaliwa za mwezi, nusu mwaka na mwaka mzima.

Sambamba na hayo aliendelea kusema kuwa pia mfumo huo utasaidia wakaguzi wa ndani kuingia na nje moja kwa moja kwenye mfumo na kuepuka utumiaji wa gharama kubwa za kuwalipa wakaguzi. 

Alisema pia mfumo huo umeunganishwa na mifumo ya kibenki, mamlaka ya mapato, taasisi za fedha za mitandao ya siku za mkononi hivyo mwanachama anaweza akafanya miamala yote bila kufika eneo husika .

“Saccos hawahitajiki kwenda TRA kufanya retain za kodi mfumo utawasaidia  kufanya retain na kulipa na gharama ya mfumo huu ni rahisi ambavyo ni laki mbili tu kwa mwaka” Alifafanua.

Aidha kwa upande wake mchumi  mwandamizi kutoka benki kuu ya Tanzania Alli Liyau alisema kuwa  kufanya kazi za ushirika bila leseni ni kosa ambapo ifikapo April 2021  wanatarajia wana saccos wote watakuwa wameshapata leseni na hakutakuwa na malalamiko.

“Kwa wale ambao bado hajaomba leseni watumie muda huu  kuhakikisha wanaomba  kwani leseni ni muhimu ili biashara ziwe rasmi” Alisema Liyau.

Alifafanua kuwa ni lazima saccos zirasimishwe ili kuweza kupata msaada pale panapotokea tatizo, pamoja na kwakuwa ni biashara ichangie mapato ya serikali kwa kulipa kodi na kuwa salama kwasababu hawatakidhana na matwaka ya serikali.

Hata hivyo maadhimisho ya siku ya vyama vya ushirika yamefanyika Mkoani Arusha na kushirikisha wanachama kutoka katika saccos elfu 6000 zilizopo hapa nchini.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: