Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya akiambatana na Meneja Utawala na Rasilimaliwatu wa Tume ya Madini, Gift Kilimwomeshi wametembelea Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Njombe lengo likiwa ni kukagua shughuli zake na kutatua changamoto za kiutumishi.
Mara baada ya kupokelewa na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Njombe, Wilfred Machumu viongozi hao wamekutana na watumishi wa ofisi hiyo na kutatua changamoto mbalimbali za kiutumishi huku wakitoa elimu na miongozo mbalimbali kwenye utumishi wa umma.
Post A Comment: