Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel,akizungumza wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel,akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Sehemu ywa wafugaji wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel,(hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi, Dk.Fatuma Mganga,akizungumza kwenye uzinduzi wa awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Katibu wa Wafugaji Kata ya Bahi Bw.Yona Paulo ,akitoa neno wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Bahi,Jeremiah Mapogo,akizungumza katika uzinduzi wa awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo, Dk.Hezron Nonga,akitoa takwimu wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Bw.Daniel Kehogo, akisoma taarifa ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof.Elisante Ole Gabriel (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel,akipokea taarifa ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Mifugo na Uvuvi Bw.Daniel Kehogo wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel,akigawa dawa za Kuogesha mifugo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Bahi, Dk.Fatuma Mganga pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya ya Bahi,Jeremiah Mapogo wakati wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel,akikata utepe kuashiria uzinduzi wa awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel,akimswaga ng'ombe kuingia kwenye maji tayari kwa ajili kuoga dawa baada ya uzinduzi wa awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel,akikagua mifugo mara baada ya kuzindua awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel,akiangalia Dume la Ng'ombe baada ya kuzindua awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo uliofanyika leo katika kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma.
..........................................................................................................
Na Alex Sonna, Bahi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof.Elisante Ole Gabriel, leo amezindua awamu ya tatu ya kampeni ya uogeshaji mifugo, huku akiwataka wafugaji nchini kuhakikisha wanaogesha mifugo ili kudhibiti magonjwa yanayoenezwa na kupe.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika kijiji cha Bahi Sokoni, Wilayani Bahi, Mkoa wa Dodoma, Prof.Elisante amesema lengo la serikali ni kuongeza toja ya ufugaji kwa kuwa na mifugo yenye afya itakayozalisha mazao zaidi yenye ubora wa kitaifa na kimataifa.
“Lengo la kuogesha mifugo ni kudhibiti magonjwa yanayoenezwa na kupe hususan Ndigana kali ambayo imekuwa ni changamoto katika kuendeleza tasnia ya mifugo nchini,”amesema.
Amebainisha kuwa magonjwa hayo yamekuwa yakiathiri mifugo na kusababisha hasara kubwa kwa mfugaji.
“Magonjwa yanayoenezwa na kupe yasipodhibitiwa ipasavyo huchangia asilimia 72 ya vifo vyote vya ng’ombe nchini, kati ya magonjwa hayo, ugonjwa wa Ndigana kali huchangia vifo kwa kiwango kikubwa cha asilimia 44,”amesema.
Katibu Mkuu huyo amesema hasara inayotokana na magonjwa hayo inakadiriwa kuwa takribani Sh.Bilioni 145, na kusababisha kupungua uzalishaji maziwa, nyama kutokana na kukonda, kushuka kwa thamani ya ngozi, kupoteza wanyama kazi na udumavu wa ndama.
Amefafanua kuwa uogeshaji wa mifugo kwa kutumia josho ni mzuri na hasa kwa wafugaji wenye mifugo mingi na unadhibiti magonjwa hayo.
Amesema mwaka 2018 Wizara hiyo ilitengeneza mkakati wa kudhibiti magonjwa hayo kwa kuanzisha kampeni hiyo ambapo kwa awamu ya kwanza na pili serikali ilinunua lita 21,373.06 zenye thamani ya Sh.Milioni 740.7 kwa ajili ya kuogesha mifugo.
“Katika awamu zote mbili kumekuwa na jumla ya michovyo Milioni 245.37 ya mifugo yote ikiwemo ng’ombe Milioni 176.32, Mbuzi Milioni 58.02, kondoa Milioni 20.03 na punda 2,685,”amesema.
Kuhusu kampeni huyo awamu ya tatu, amesema serikali imenunua dawa ya kuogesha mifugo aina ya Paranex, Paratop, Amitraz kiasi cha lita 15,579 zenye thamani ya Sh.Milioni 592.82 ambazo zitatosheleza majosho 1,983 katika halmashauri 162 na michovyo inayotarajiwa ni Milioni 405 ya mifugo yote itakayoogeshwa.
Ameagiza Halmashauri kusimamia kanuni ya uogeshaji ili wafugaji waifuate na kushirikiana nao na wadau kujenga na kukarabati majosho yake na miundombinu mingine ya mifugo.
Awali, akitoa taarifa ya uogeshaji mifugo wilayani Bahi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Dk.Fatuma Mganga, amesema mifugo inachangia zaidi ya asilimia 55 ya mapato ndani ya Halmashauri hiyo kwa mwaka.
Amesema kuna minada 15 ambayo hufanyika biashara ya kuuza wastani wa ng’ombe 3,882, mbuzi 4,602 na kondoo 89 kwa mwezi.
Hata hivyo, amesema halmashuari imekwisha andika andiko la mradi wa kiwanda cha uchakataji ngozi lenye thamani ya Sh.Bilioni 3.3 tayari andiko hilo lipo Wizara ya Fedha kwa ajili ya mapitio ya mwisho kabla fedha kutolewa.
Naye, Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo, Dk.Hezron Nonga, amesema mwaka 2019, majosho zaidi ya 511 yalikarabatiwa nchi nzima kwenye Halmashauri huku 78 mapya yalijengwa.
“Vifo vya ng’ombe hususan ndama vilipungua kwa asilimia 30 kwasababu ya uogeshaji, tukiogesha vifo vya ng’ombe zetu tunatokomeza,”amesema.
Post A Comment: