Na Esther Macha,Mbarali
MGOMBEA ubunge Jimbo la mbarali kupitia CCM ,Francis Mtega amewaomba wananchi wa kijiji cha chalisuka katika kata ya Madibira kumchangua ili aweze kuwawakilisha bungeni ikiwa ni pamoja na kushirikiana katika kutatua kero zinazowakabili.
Mtega amesema hayo leo wakati wa mwendelezo wa mkutano wa kampeni wa kunadi sera za chama cha mapinduzi katika kijiji cha Chalisuka .
Aidha Mtega amesema kuwa hataweza kufanya vizuri pekee iwapo hawatamchagulia diwani wa CCM .
"Nichagueni kwa kura nyingi naamini kuwa nitashirikiana na wenzangu hivyo najua Madibira mtapiga hatua kubwa ya kimaendeleo, CCM pekee ndo wanaobeba ilani ya uchaguzi kwa miaka mitano yenye mambo mengi ya kimaendeleo"alisema.
Aidha Mtega alisema mh Rais anaenda kufanya mambo yote ya msingi na kuwa endapo mtachagua chama kingine watambue kuwa watakuwa wamezuia maendeleo naombeni wekeni mnyororo wa maendeleo ambao ni Rais,Mbunge,Diwani.
Post A Comment: