Na Esther Macha,Mbarali

ZIKIWA zimesalia siku chache Watanzania wametakiwa kutumia  haki yao ya kikatiba kwenda kupiga kura October 28 mwaka huu ,Mgombea ubunge wa Jimbo la Mbarali Francis Mtega  kupitia CCM ameendelea  kunadi sera zake  katika kata za jimbo hilo.


Akiwa kata ya Ipwani katika vijiji vya Lemsemi ,Ibelege,Matemela ,Mtega amesema kuwa ili Jimbo la Mbarali liwe mna maendeleo  wanancghi  wamchague Dkt.Magufuli ngazi ya urais, yeye Mbunge na Diwani wa chama cha mapinduzi.


Aidha Mtega alisema kuwa katika kutatua kero  za wananchi atawakilisha kwero za wananchi kwa Mawaziri  mbali mbali moja kwa moja pamoja na kuwawakilisha kwa Rais Magufuli ili waweze kutatua changamoto za wananchi .


“Nipeni ridhaa ya kuwa Mbunge wenu ili niweze kutatua changamoto zenu ambazo zinawakabili ndugu zangu ,nipo tayari kuwatumikia wananchi nipeni nafasi muone jinsi ambavyo nitashughulikia changamoton zenu ,pale itakapobidi nitatumia  fedha kutoka mfukoni mwangu “amesema Mtega.


“Nafahamu sana changamoto za hapa Ipwani maana nimekuwa Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya mbarali  kwa miaka mitano najua hapa mna shida ya maji na mmeomba kuchimbiwa visima vya  maji pamoja changamoto kubwa ya maji ,nipeni ridhaa niweze kuwasaidia kutatua changamoto hizi “amesema Mtega.


Kwa upande wake Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mbarali ,Suleiman Kondo ambaye ameongozana na mgombea huyo kumnadi aliwataka wana Ipwani kumpa nafasi mgombea wa ccm kwani ni mtu ambaye  ni msikivu .


Mwisho.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: