Mgombea udiwani kata ya Sekei kupitia chama cha mapinduzi CCM Gerald John Sebastian ameawaahidi wananchi  endapo watamchagua Rais John Pombe Maghufuli  kuwa rais wa nchi kwa mara nyingine, Mrisho Gambo kuwa Mbuge jimbo la Arusha mjini nayeye kuwa diwani wa kata hiyo atawatumikia masaa 24 bila kuchoka.


Sebastian aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni zake katika kata hiyo ambapo ameeleza kumekuwa na changamoto nyingi zilizokosa ufumbuzi kwa muda mrefu katika kata hiyo ikiwemo, ujenzi wa shule ya sekondari ya kata.  


“Mkinichagua nawahakikishia mtakuwa mmelamba dume, kwani maendeleo yote mliyotakiwa kuyapata miaka kumi mliyowapa upinzani miaka kumi, mimi ndani ya miaka mitano nitaweza kuwafanyia kwa kutekeleza ilani ya Ccm” Alisema Gerald Sebastian.


Alieleza kuwa ni jambo la aibu kata hiyo yenye ofisi nyingi za serikali kutokuwa na shule ya kata jambo ambalo limetokana na kuwapa uongozi watu ambao sio sahihi ambapo wakimchagua yeyea atashirikiana na wananchi pamoja na viongozi wa serikali kuhakikisha  maendeleo yanapatikana kwa haraka .


“Nitajitoa masaa yote kwaajili ya kuhakikisha natatua kero zinzowakabili na pia naanza kufanya kazi kwanzia sasa hivi hata kabla hamjanichagua” alisisitiza


Kwa upande wake mgombea ubunge jimbo la Arusha mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi Mrisho Gambo alisema amebakiza kata tatu amalize kata zote za jimbo hilo kufanya mikutano ya hadhara na atabadili  ya ufanyaji wa kampeni.


"Tumefanya mikutano zaidi ya kata 20 na hizi tatu zilizo baki tukimaliza  tunaanza kampeni za nyumba kwa nyumba, mlango kwa mlango na ikibidi kitanda kwa kitanda"alisema Gambo


Awali aliwaomba wakazi wa kata hiyo kukipigia kura chama cha mapinduzi kwa staili ya mafiga matatu yaani diwani, mbunge na Rais ili iwe rahisi kupenyeza hoja za  vipaumbele vya jimbo lake.


Hata hivyo mgombea huyo wa kiti cha udiwani alipewa ilani ya chama chake kwa lengo la kwenda kuitekeleza endapo atapata ridhaa ya wananchi.


Mbali na hilo wagombea hao walivishwa mashuka ya kimasai lakini pia walipewa fimbo kama ishara ya usimamizi na uongozi kwa kabila hilo ambalo ndio wenyeji wa mkoa wa Arusha.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: