Mbunge Mteule wa Viti Maalumu (CCM) Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira akizungumza na timu za Kisayansi Kata ya Nshambya
Mbunge Mteule wa Viti Maalumu (CCM) Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira katikati akiwa kwenye picha na timu ya Kisayansi ya Kata ya Kahororo
Mbunge Mteule wa Viti Maalumu (CCM) Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira akiwa kwenye picha ya pamoja na timu ya Kisayansi Mtaa wa Kisindi kata ya Kashai
Mbunge Mteule wa Viti Maalumu (CCM) Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira akiwa kwenye timu ya pamoja na timu ya Kisayansi Kata ya Nshambya na Mgombea Ubunge alifika kusalimia ,Adv Byabato
TIMU ya Kisayansi ya Mtaa wa Kashenye Kata ya Kashai
TIMU ya Kisayansi ya Wazee Mashuhuri kutoka Kijiwe cha Senet,Soko Kuu na Bukoba wakiwa na |
Mbunge Mteule wa Viti Maalumu (CCM) kundi la Asasi za
Kiraia (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira amekutana na Timu za
Kisayansi zote nne alizoziunda kutoka mitaa 10 ya Jimbo la Bukoba Mjini
ambayo yeye ni Mlezi wa Uchaguzi wa CCM. Timu hizi zina wajumbe wa
kimkakati na uwakilishi wa makundi yote muhimu.
Lengo
la kukutana ilikuwa kujitathimini na kupelekea mipango ya kisayansi
itakayo wezesha ushindi wa kishindo wa CCM kuanzia ngazi ya Urais,
Ubunge na Udiwani Octoba 28 mwaka huu.
Akizungumza
Neema alisema ili kufanikisha lengo kuratibu ushindi kwa CCM kwenye
mitaa 10 kwa kutumia ubunifu aliamua kuunda timu za kisayansi 4 kutoka
makundi yote muhimu .
“Timu
hizo zina jumla ya watu 140 wa kimkakati ambao kwa kushirikiana na
Lugangira wanaratibu kazi ya kisayansi kwa maeneo ya kisayansi na Octoba
9 na 10 mwaka huu nimekutana na timu zote nne kwa lengo la
kujitathamini” Alisema
Pamoja
na Timu hizi 4 za Kata, Lugangira pia aliunda Timu ya Kisayansi ya
Wazee 15 Mashuhuri kutoka Kijiwe cha Senet, Soko Kuu Bukoba Mjini ambao
pia alikutana nao tarehe 8 Oktoba 2020 na kupata tathmini ya majukumu ya
kisayansi aliyowakabidhi.
Aidha
alisema pia lengo lingine la Mikutano hii ilikuwa ni kuweka mipango ya
kisayansi itakayopelekea ushindi wa kishindo wa Chama cha Mapinduzi kwa
ngazi ya Rais, Ubunge na Udiwani katika uchaguzi huo.
“Kwa
Kampeni yetu ya Kisayansi lazima Wilaya ya Bukoba Mjini ichukue nafasi
yake ya kuwa sebule ya Mkoa wa Kagera", Alisisitiza Lugangira.
Post A Comment: