NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Kikundi cha mazoezi(Arusha Jogging club) kilichoanzishwa takriban miezi miwili sasa na mkuu wa wilaya ya Arusha Kennan Kihongosi kimekuwa msaada kwa watu wenze uzito mkubwa pamoja na unene uliopitiliza walioweza kuhudhuria mazoezi hayo.
Akizungumza wakati wa mazoezi hayo Fatma Kibola alisema kuwa kabla ya kuanza mazoezi hayo alikuwa na uzito wa kilo 120 ambapo kwa sasa ana kilo 110 na anategemea akiendelea kuhudhuria kilo zake zitazidi kupungua na kumfanya awe na furaha zaidi.
“Mazoezi haya yamenisaidia sana naadha kuona mwili wangu unapungua uzito siku hadi siku sasa hivi Nina kilo 110 na natarajia ninavyoendelea na mazoezi haya nitazidi kupungua kwani ndicho ninachokitaka kwa sasa, nikipunguza uzito nitakuwa na furaha” Alisema Bi Kibola
Sindi Kasambala amewahimiza akina mama waliopo majumbani wanaaumbuliwa na magonkwa mbalimbali kuhurudhuria mazoezi hayo ambavyo yatawafanya wawe na afya mzuri kwani amewaona mabinti wadogo wengi huku akina mama wakiabaki majumbani.
“Katika mazoezi haya nawaona mabinti wwngi wadogo huku akina mama wenye umri mkubwa ambao baadhi yao wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali ikiwemo uzito mkubwa na vitambi wakibaki majumbani nawasii wahudhurie mazoezi haya watapata nafuu”
Alisema Sindi Kasambala.
Aidha mmoja wa walimu wa mazoezi hayo aliyejitambulisha kwa jina la Hansi aliwataka wanamazoezi wote kuwahi ili waweze kumaliza mapema, walimu wapate fursa za kufundisha vizuri kila mmoja kulingana na utaalamu wake ikiwa ni pamoja na washiriki wote kuhakikisha wanavaa kimazoezi wanapokuwa katika mazoezi hayo.
“Vaaeni kimazoezi, msivae viatu vya wazi unaweza kukanyagwa bahati mbaya ukaanguka ukianguka mmoja unaweza sababisha hata zaidi ya watu kumi wakaanguka kwahiyo ni hatari mwanamazoezi kuvaa viatu vya wazi vaeni raba”
Kwa upande wake wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi alifafanua kuwa lengo la kuanzisha clabu ya ufanyajiwa mazoezi kila siku ya jumamosi ni ili kutengeneza amani, umoja na mshikamano kwani vijana wanapokuwa kitu kimoja wana nguvu kubwa ya kufanya maendeleo ya pamoja.
Kenan alisema kuwa yeye kama mkuu wa wilaya jukumu lake ni kuwaunganisha vijana ambapo ametoa wito kwao kulinda amani na utulivu uliopo ndani ya wilaya ya Arusha ikiwa ni pamoja na kuhudhuria ka wingi katika mazezi hayo kwani mazoezi ni afya, furaha na upendo.
“Tulianza tukiwa 14 lakini hivi sasa Tupo zaidi ya 150 na tunashirikiana pia na vilabu mbalimbali wakiwemo Arusha runners, Atras, Vitambi noma na wengine wengi hivyo nawakaribisha na watu wengine wake kila jumamosi saa 12 kamili tuje kutengeneza miili yetu lakini pia kujenga umoja na kutumia amani iliyopo” Alisema Kennan Kihongosi.
Naye mmoja wa wankamati wa mandalizi ya mazoezi hayo Gerald Sebastian ambaye pia ni mgombea udiwani wa kata ya Sekei kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi [CCM] alieleza kuwa pamoja na mazoezi hayo pia kutakuwa na tukio la kuwajumuisha wanamazoezi hao kwaajiliya kufurahi pamoja na kuzungumzia masuala ya uchaguzi.
“Vijana wa Arusha wamesahaulika katika suala zima la kupata elimu huu ya masuala ya siasa kwahiyo pamoja na mazoezi haya tutakuwa na siku ya kufurahia na kuzungumza masuala mbalimbali ikiwemo kufahamiana na kuzungumzia masuala ya siasa hasa ukizingatia tunaelekea katika uchaguzi mkuu October 28 mwaka huu.
Post A Comment: