Na John Walter- Manyara
Mgombea Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Magufuli amesema kitendo cha Waziri Mkuu wa awamu ya tatu, Fredrick Tluway Sumaye na Mbunge mteule wa Jimbo la Babati Mjini Pauline Gekul kuondoka CCM na kuhamia upinzani ni sawa na kushikwa na mapepo lakini sasa roho mtakatifu amewashukia na kurudi CCM.
Amefananisha kitendo hicho cha Sumaye kuhama CCM na kujiunga na upinzani ni sawa na tukio la Malaika waliomuasi Mungu na kutupwa duniani.
Dkt Magufuli ameyasema hayo mjini Babati Mkoani Manyara kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Kwaraa.
Amesema Sumaye ni mwana CCM halisi aliyepotea kwa bahati mbaya kutokana na mapepo yaliyomkumba siku za nyuma pamoja na Mgombea Ubunge Jimbo la Babati Mjini, Paulina Gekul ambaye awali alikuwa CHADEMA.
Amesema Waziri mkuu huyo mstaafu alijifunza mapema akawakimbia na sasa amerudi CCM kwani kiongozi mwadilifuna hicho chama hakikumfaa, kwani kinasimama hadharani na kumtukana kila mmoja na hakina staha.
“Ninamshukuru roho mtakatifu aliyekugusa Mzee Sumaye na ukarudi nyumbani, kufanya kosa siyo kosa, kosa ni kurudia kosaa na ninatambua umefika nyumbani hongera Mungu akubariki na uzao wako.
Hata hivyo, amesema pamoja na kuomba ridhaa ya kuendelea kuongoza nchi, urais ni kazi yenye mateso makubwa.
Amewaomba Watanzania wamchague tena Oktoba 28 ili amalizie kazi alizozianza katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Amesema baada ya hapo watachagua wengine ingawa ana uhakika atakuwa wa CCM kwa kuwa mazingira wameweka vizuri na wamejitahidi kuhakikisha nchi inasonga mbele.
Hata hivyo, amesisitiza umoja na mshikamano kuendelea kutawala nchini ili kuweza kusukuma gurudumu la maendeleo na wasikubali kugawanywa na watu wasio na nia njema.
Post A Comment: