Viongozi wa Jumuiya ya Watumia Maji wa Bwawa la Nhumbu Mkoa wa  Shinyanga waliochaguliwa juzi mkoani humo wakiwa katika picha ya pamoja. Kutoka kulia ni  Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Ndoshi Magadula, Mwenyekiti Msaidizi, Ndula Maboma, Katibu, John Boniphace, Mtunza Hazina,  Eunice Machiya, Mjumbe, Anastazia Mihambo na Mjumbe, Majiku Salumu. 

Afisa Maendeleo  ya Jamii Mkuu Bodi ya Maji Bonde la Kati, Halima  Faraji, akizungumza katika uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya ya Watumia Maji wa Bwawa la Nhumbu Mkoa wa  Shinyanga waliochaguliwa juzi mkoani humo.

Afisa Maendeleo  ya Jamii Mwandamizi wa Bodi ya Maji Bonde la Kati, Nelea Bundala, akizungumza katika uchaguzi huo.

Kura zikihesabiwa.

Kura zikihesabiwa.
Mchakato wa uchaguzi ukiendelea. Kulia ni Afisa Maendeleo  ya Jamii Mwandamizi wa Bodi ya Maji Bonde la Kati, Hhau Sarwatt, akishiriki uchaguzi huo. Kutoka kushoto ni Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye pia ni Afisa Uvuvi kutoka Wilaya ya Kishapu. Moses Zacharia, Afisa Mazingira kutoka Kampuni ya Williamson Diamonds Limited, Queen Tizeba na Fundi Sanifu kutoka Ofisi Ndogo ya Bonde la Kati- Shinyanga, Israel Chafumbwe.
Uchaguzi ukiendelea.
Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye pia ni Afisa Uvuvi kutoka Wilaya ya Kishapu. Moses Zacharia, akitangaza matokeo. .
Watendaji wa kata na wenyeviti wa vijiji wakiwa kwenye uchaguzi huo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwigumbi Kata ya Mondo, Sospeter Mapinda, akizungumza kwenye uchaguzi huo.
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Seseko, Hamis Ndege, akizungumza kwenye uchaguzi huo.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Mondo, Masanja Said, akizungumza kwenye uchaguzi huo.
Mhandisi kutoka Kampuni ya Williamson Diamonds Limited, Raphael Matola akizungumza kwenye 
uchaguzi huo.
Afisa Kilimo kutoka Manispaa ya Shinyanga Daniel Nsanzugwanko, akizungumza kwenye uchaguzi huo.
Fundi Sanifu wa Umeme na Vifaa vya Umeme wa Wakala wa Maji Safi na Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Kishapu, Christopher Damas, akizungumza kwenye uchaguzi huo.
Picha ya pamoja baada ya uchaguzi huo.
Picha ya pamoja baada ya uchaguzi huo.


Dotto Mwaibale na Godwin Myovela, Shinyanga.


JUMUIYA ya Watumia Maji wa Bwawa la Nhumbu Mkoa wa  Shinyanga imepata viongozi wake kwa mara ya kwanza baada ya kufanyika uchaguzi  ambapo watahudumu katika nafasi zao kwa muda wa miaka mitatu.

Uchaguzi huo ulifanyika juzi eneo la Songwa nje kidogo ya Manispaa ya Shinyanga na kuhudhuriwa na watendaji wa kata na wenyeviti wa vijiji wanaotumia maji ya Bwawa hilo ambalo jumuiya hiyo itakuwa na jukumu la kulilinda.

Uchaguzi huo uliandaliwa na Bodi ya Maji Bonde la Kati ambao walitembelea vijiji nane na kufanya mikutano ya hadhara ya kuwapata wajumbe watatu kutoka katika kila kijiji ambao wameunda jumuiya hiyo kwa kuzingatia jinsia na makundi ya wafugaji, wakulima na watumiaji wa maji.

Baada ya mikutano hiyo Bodi ya Maji Bonde la Kati ilitoa mafunzo ya siku tatu kwa wajumbe hao na kuunda jumuiya hiyo yenye lengo la kujua wajibu wao na namna ya kulinda rasilimali za maji.

Katika uchaguzi huo Ndoshi Magadula alichaguliwa kuwa Mwenyekiti kwa kupata kura 16 sawa na asilimia 7 huku nafasi ya Mwenyekiti Msaidizi ikichukuliwa na Ndula Maboma ambaye alipata kura 5 sawa na asilimia 20.8.

Nafasi ya Katibu ilikwenda kwa John Boniphace ambaye alipata kura 22 sawa na asilimia 91.7 huku Eunice Machiya akichaguliwa kuwa Mtunza Hazina  kwa kupata kura 16 sawa na asilimia 66.7.

Katika uchaguzi huo walichaguliwa wajumbe wawili ambao ni Anastazia Mihambo ambaye alipata kura 15 sawa na asilimia 62.5 na Majiku Salumu aliyepata kura 16 sawa na asilimia 66.7.

Akizungunza kwa niaba ya wenzake Magadula alisema watashirikiana na wana jumuiya hiyo na kuhakikisha kila kilichokusudiwa kinakwenda sawa ikiwa ni pamoja na kulinda rasilimali  za maji katika eneo hilo hasa Bwawa la Nhumbu. 

Share To:

Post A Comment: