NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA


Viongozi wa jumuiya ya maridhiano wamewataka wananchi kujiepusha na makundi yanayotishia amani hasa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu Octoba 28 mwaka huu.


Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha ,Katibu Mkuu mwenza wa jumuiya hiyo Shekhe Abdulrazak Amiri alisema katika kipindi hiki cha uchaguzi ni vyema watanzania wakalinda amani ya nchi kwani ikitoweka  shughuli za maendeleo zitasimama kutokana na machafuko ambayo yanaweza kuletwa kwa ukabila ,dini na siasa.


Shekhe Amiri ametoa rai kwa viongozi wa dini kutovaa nguo zinazoashiria kukiunga chama chochote cha siasa kwani haileti picha nzuri ikiwa wajibu wa kiongozi wa dini ni kupigania amani na kukemea vitendo vyovyote vinavyoashiria uvunjifu wa amani.


"Sisi watanzania tupambane kulinda amani yetu kwani kuna baadhi ya nchi hazina amani na shughuli zote zimesimama hivyo tusikubali wachache wavuruge kwakuwa amani ikishaondoka, uhuru wakufanya maendeleo tulionayo sasa tutaikosa,"alisema katibu huyo.


Kwa upande wake mwenyekiti wa maridhiano mkoa wa Arusha Askofu Dk.Jackob Shega alisema katika kipindi hiki cha uchaguzi kumekuwa na kumekuwa na kampeni za kila mgombea kunadi sera zake ili apate kibali cha kuchaguliwa na wananchi hivyo ni vyema kila mmoja akakubali matokeo yatakayokuja na washirikiane kwa kuleta maendeleo ya nchi kwa pamoja.



"Watakao pata nafasi ya kuchaguliwa na ambao kura zao hazitatosha kwasababu mwisho wa siku ni lazima kila eneo apatikane mtu mmoja wa kuongoza, kubalianeni na matokeo lakini pia mshirikiane na kuleta maendeleo hivyo watanzania wote tuwe na malengo ya pamoja katika kulinda amani yetu isiharibiwe na wachache,"alisema Mwenyekiti huyo.



Alieleza kuwa watanzania wote  ni vyema kutanguliza amani,upendo na ushirikiano ikiwa amani ni tunu ya Taifa letu kwani mwisho wa uchaguzi kuna athari zinazoweza kutokea kutokana na mtu kutoridhika na matokeo  hivyo ni vyema tukajiepusha na makundi ambayo hayajali amani yetu.


Askofu Shega alisema ni vyema wazazi wakawaasa vijana wao kuzingatia amani katika kipindi hiki cha uchaguzi kwani wangependa baada ya uchaguzi amani na mshikamano viendelee na wafahamu kuwa Tanzania ndo nyumbani.



Naye Fatuma Hasan mjumbe wa jumuiya hiyo aliwasihi wanawake wote kuzungumza na vijana wao na kuwaomba kutokujiingiza kwenye magenge ambayo mabaya yenye malengo ya kuharibu amani ya nchi.


“Kama mama nawasihi vijana wasishawishike na jambo lolote lenye viashiria vya kuvuja amani kwani amani hii wanayoifaidi hivi sasa kuna wazee wao ambao waliitafuta” alisisitiza Fatuma  Hasan.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: