NA NAMNYAK KIVUYO ,ARUSHA

Mkurugenzi wa halmashauri ya  jiji la Arusha Dr John Pima amewataka wafanyabishara zaidi ya 1800  wa soko kuu la Arusha, Kilombero, stend kubwa pamoja na stend ndogo kuendelea na biashara zao kama kawaida bila kuwasikiliza wanaopotosha juu ya tenda kwani tenda zilitangwazwa July mwaka huu zimefutwa ili kusubiri maamuzi ya baraza la madiwani.

Dr Pima aliyasema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari baada ya kupata taarifa kuwa kuna watu wanaojiita mawakala wa wafanyabiashara na madalali wanaowarubuni watu kuwa tenda hizo zipo.

Alifafanua kuwa tenda iliyotangazwa July mwaka huu iliondolewa ili kusubiri maamuzi ya baraza la madiwa linalotarajiwa kukutana December mwaka huu hivyo wafanyabiashara wafanye kazi zao kwa uhuru na kwa bei ile ile waliyokuwa wakilipa miaka yote.

“Mnaowapotosha wananchi acheni, na ikitokea kwanzi sasa anyepotosha juu ya tenda wafanfanya biashara ripotini hapa almashaurj au kwa jeshi la polisi ”Alisisitiza Dr Pima.

Aidha aliwataka wote walioshinda tenda katika maduka mapya 67 kati ya 100 nje ya yale 1800 ambazo tenda zake zimefutwa kuendelea na biashara na taratibu ambazo hawajazilamilisha kwani maduka hayo hayana mgogoro wowote.

“Halmashauri imejenga maduka mapya 100 ambapo maduka 67 yameshapata wapangaji  ambao baadhi wameshakabidhiwa funguo na wengine wakiendelea na mchakato wa kukamilisha taratibu”

Aidha alisema kuwa hakuna mgogoro wowote kati ya wafanyabiashara na halmashauri lakini kuna suala la wajenzi wa maduka hayo ambapo  wameshaongea nao na wenyewe wanasubiri maamuzi ya baraza la madiwani.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: