NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Arusha mjini Dr John Pima amewataka wananchi wa Jimbo hilo kufuata taratibu na maelekezo watayopewa na wasimamizi wa vituo ili kuweza kukamilisha zoezi hilo kwa utulivu na amani.
Dr Pima alitoa rai hiyo wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na maendeleo ya maandalizi ya uchaguzi ambapo alisema kuwa vituo vitakuwa wazi kwanzia saa moja kamili asubuhi hivyo wananchi wawahi na kuangalia chumba wanachopaswa kupigia kura, kujianga pamoja na kufanya zoezi hilo.
“Wananchi nawasihi mbebe vitambulisho vyenu vya kupigia kura, lakini pia kama umekipoteza na taarifa zako zipo katika daftari la mpiga kura beba kitambulisho cha taifa au leseni ya udereva na utaweza kupiga kura bila usumbufu wowote”alisema Dr Pima.
Alieleza kuwa baada ya kufuata maelekezo na kuweza kupiga kura, wananchi warudi majumbani mwao na kusubiri matokeo baada ya zoezi hilo kukamilika kwa watu wote watakaofika kituoni na ifikapo saa kumi jioni vituo vitafungwa lakini wote watakaokuwa vituoni watapiga kura.
Aidha alifafanua kuwa mawakala wa vyama vya siasa ambao watahusika katika zoezi la uwakala niwale tu ambao
time inawatambua kwa maana ya waliofuata taratibu zote zilizohitaji na kuweza kukidhi vigezo ambapo pia wagombea wa udiwani na Ubunge watakaoruhisiwa kuingia katika vyumba vya majumuisho ni wale tu ambao wamekula kiapo cha uwakala.
Pia alifafanua kuwa mwisho wa kampeni ni leo October 27 saa 12 kamili na matangazo ya vyama mwisho ni saa mbili kamili usiku pamoja na kuwataka wananchi, wagumbea na wafuasiwa vyama mbalimabali kutoenda katika vituo vya kupigia kura wakiwa wamevaa nguo zinazowakilishavyama.
Sambamba na hayo pia akiwataka viongozi wa vyama vya siasa kujiepusha na mihemko ya kutoa taarifa zozote za matokeo kwani jukumu hilo sio la kwao na endapo watafanya hivyo watakuwa wamevunja Sheria na kusema kuwa tume imejipanga kutenda haki na sio vinginevyo.
Hata hivyo vyama vitakavyoshiriki zoezi la uchaguzi katika Jimbo la Arusha mjini ni vyama 15, wapiga kura laki 374,000, vituo 910 huku kukiwa na waangalizi wa ndanina nje 18 ambao wote wametakiwa kuzingatia maadili na miiko waliyopewa.
Post A Comment: