………………………………………………………………………………………..
Mgombea Ubunge wa Mbeya Mjini kupitia CCM Dr. Tulia Ackson ameendelea na ziara zake za kampeni kuelekea Uchaguzi mkuu wa October 28, 2020 na leo kituo kikuu kilikuwa katika kata ya Iziwa jijini humo ambapo amewaeleza Wananchi hao kwamba miongoni mwa sababu zilizompelekea kuomba ridhaa ya kuwatumikia ni pamoja na kutaka kulibadilisha Jimbo hilo kuwa na maendeleo ya kiuchumi, kielimu, afya pamoja na miundombinu.
“Leo nitawaeleza ni kwanini tunasema Mchagueni Magufuli awe Rais wetu na Tulia awe Mbunge wa Mbeya mjini, katika Ilani yetu ya mwaka 2020-2025 imeeleza ni namna gani tunakwenda kuibadilisha Mbeya Mjini endapo mtatupa nafasi ya kuwatumikia, CCM kazi yetu ni kuleta maendeleo kwa Wananchi wake na wala hatuna tamaduni za kutoa matusi kwamaana sisi tunasikilizwa na kila rika wakiwemo wazee na watoto”- Dr. Tulia Ackson
“Hapa nimewaona watoto wa shule ya msingi Iziwa, labda nianzie hapohapo kuwaeleza jambo kwamba mimi Mbunge wenu wa kujiongeza hata kabla hamjanipa nafasi nilishakwenda pale na nikatoa msaada wa mifuko 100 ya Cement ili kuwezesha ujenzi wa choo ambacho kilikuwa katika mazingira mabovu alafu nasikia kuna mtu anajinasibu kwamba ni yeye aliyeifanya kazi hiyo, safari hii hawa watu tunasukuma nje”- Dr. Tulia Ackson
“Hapa kwenye kata yetu ya Iziwa kuna ukosefu wa shule ya Sekondari licha ya kuwepo kwa eneo, sasa kazi ni ndogo tu kwenu ambapo mnachotakiwa ni kuchagua viongozi wote wa kutoka CCM muone kitakachoenda kufanyika hapa na tayari ushahidi mmeanza kujionea wenyewe hata kabla hamjatuchagua”- Dr. Tulia Ackson
“Kwenye upande wa miundombinu, barabara yetu hii ya kutoka Mbata inayopita Nonde kuelekea Nsoho hadi mtaa wa Isengo yote ni vumbi tupu, sasa ndugu zangu hii tukitaka ikae vizuri lazima tumchague Magufuli, ni lazima tumchague Tulia ambaye anauwezo wa kumuambia Rais Magufuli kuhusu changamoto zetu na akazitatua”-Dr. Tulia Ackson
Post A Comment: