Mkuu
wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof.Eliamani Sedoyeka, akizungumza na
waandishi wa habari leo wakati akitangaza kuwa chuo hicho kinatarajia
kuanza ujenzi wa tawi lake jijini Dodoma.
Mkuu
wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof.Eliamani Sedoyeka, akisisitiza jambo
kwa na waandishi wa habari leo wakati akitangaza kuwa chuo hicho
kinatarajia kuanza ujenzi wa tawi jipya jijini Dodoma kulia ni Mkuu wa
kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Fedha na Mipango Benny
Mwaipaja.
Sehemu
ya waandishi wa habari wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Chuo cha Uhasibu
Arusha Prof.Eliamani Sedoyeka,(hayupo pichani)wakati akitangaza kuanza
kwa ujenzi wa tawi jipya la chuo hicho jijini Dodoma.
Maafisa kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha wakifatilia Mkutano huo.
Mipango Benny Mwaipaja,akizungumza na waandishi wa habari leo jijini
Dodoma wakati Chuo cha Uhasibu Arusha kinatangaza kuanza ujenzi mpya wa
tawi lake.
Mkuu
wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof.Eliamani Sedoyeka,akiwa katika picha ya
pamoja na maafisa wa chuo hicho mara baada ya kuzungumza na waandishi
wa habari kuhusu ujenzi wa chuo hicho jijini Dodoma.
Mkuu
wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof.Eliamani Sedoyeka,akiwa katika picha ya
pamoja na waandishi wa habari mara baada ya kuzungumza nao kuhusu
ujenzi wa chuo hicho jijini Dodoma
......................................................................................................
Na Alex Sonna ,Dodoma
CHUO
cha Uhasibu Arusha(IAA), kinatarajia kufungua tawi lake Jijini Dodoma
Desemba mwaka huu kwa ajili ya masomo ngazi ya shahada ya uzamivu na
mafunzo ya muda mfupi kwa mawakala wa benki na wanaoendesha huduma za
fedha kwa njia ya simu.
Akizungumza
leo na waandishi wa habari Jijini Dodoma, Mkuu wa Chuo hicho,
Prof.Eliamani Sedoyeka, amesema kitaanza kutoa masomo hayo kwenye jengo
la kupanga huku wakitarajia kuanza ujenzi wa majengo yao Januari 2021
kwenye eneo la Njedengwa.
Amesema
kuwa hatua hiyo inatokana na nusu ya wanafunzi wa shahada ya uzamivu
kuwepo Dodoma, hivyo Chuo kinafungua tawi hilo ili kurahisisha utoaji
elimu na kuunga mkono jitihada za serikali kuhamia Dodoma.
Prof.Sedoyeka amesema watajenga kwa kutumia utaratibu wa ‘force account’ ili kuanza kutoa mafunzo kuanzia ngazi ya astashahada.
Kuhusu mafunzo ya muda mfupi, Mkuu huyo amesema yatatolewa kwa wiki
sita na yanalenga kuchochea masuala ya kiuchumi ili kuwepo na uchumi
shirikishi wenye weledi na ujuzi.
Amebainisha
kuwa katika Mpango Mkuu wa Maendeleo Sekta ya Fedha nchini wa miaka 10,
Taasisi za elimu ya juu nchini na taasisi za utafiti zimeagizwa kutumia
fursa zilizo kwenye mpango huo ili kujipanga katika kuboresha maeneo ya
kitaalamu na kiutafiti ili sekta iendelee kukua na kuhimilia ushindani
na mabadiliko.
“Kwenye
Mpango kuna maagizo kwenye taasisi za elimu ili kufanikisha kufikia
malengo hayo, tukaamua kuanzisha course za muda mfupi ambazo zitakuwa za
wiki sita kwa Agent Banking na Mobile money kutokana na sekta hii ndio
inaonekana kukua kwa kasi lakini watoa huduma hawana utaalam
huo,”amesema.
Amesema
sekta hiyo inakua kutokana na uwekezaji wa serikali kwenye masuala ya
mawasiliano na upatikanaji wa umeme ambapo huduma hizo zipo hadi maeneo
ya vijijini hivyo mafunzo hayo yatakuwa ya muhimu kwao kuwa wabobezi
kwenye utoaji wa huduma hiyo.
“Ili
kuendana na jitihada za serikali tumejipanga kutoa mafunzo haya ambayo
yatawafikia moja kwa moja watanzania, hii sekta ndogo ya fedha sio ndogo
kama tunavyofikiri ndio eneo ambalo watanzania wengi kwasasa wanatumia,
tunaamini hatua hii itasaidia kutambua biashara hiyo lakini pia kujua
namna ya kuiendesha,”amesema.
Ameeleza kuwa mafunzo hayo kwasasa yatatolewa Arusha, Dar es salaam na Dodoma na baadaye yataenda kwenye maeneo mengine.
Post A Comment: