NA MWANDISHI WETU, PANGANI

MWENYEKITI wa Chama Cha wafugaji Tanzania (CCWT) Jeremia Wambura ameagiza katibu wa chama hicho wilaya ya Pangani Chirstopher Benedict kukamatwa mara moja kwa kosa la kuuza ng'ombe 41 na mbuzi 38 waliochangwa na wafugaji wa kata  ya  Bushiri kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya  madarasa ya kidato cha tano na cha sita kwenye sekondari ya kata hiyo.


Aidha mkuu wa wilaya ya Pangani  Zainabu Issa  Machi 22,  2017 alifanya harambee ya ujenzi wa madarasa hayo ambapo wafugaji walileta mifugo yao hiyo ili iuzwe na fedha zitakazopatikana zielekezwe kwenye mradi huo wa madarasa.



Wambura alitoa agizo hilo jana kwenye mkutano wa hadhara wa wafugaji wa wilaya hiyo uliokuwa na lengo la kusikiliza changamoto zinazowaoabili wafugaji hao.


"Hawezekani wafugaji wachange mifugo yao kwa ajili ya ujenzi wa madarasa halafu mtu mmoja achukue mifugo hiyo na kuiuza kwa maslahi yake binafsi hii hakiubaliki.Dustan asakwe popote alipo ahojiwe kwa kina ataje wenzake wote waliohusika kuuza mifugo hiyo  na ikibidi afikishwe mbele ya vyombo vya sheria".


Kwa mujibu wa Wambura amepata taarifa kuwa  mifugo hiyo ilichukuliwa na katibu huyo na kupelekwa kwenye moja ya mnada  ulioko wilaya ya korogwe licha ya wilaya ya Pangani kuwa na minada ni dhahiri kuwa kuna hujuma za kutaka kumchonganisha mkuu wa wilaya na wafugaji.


"Mkuu wa wilaya amefanya kazi nzuri ya kuhakikisha watoto wetu wa kifugaji wanapata elimu bora halafu mtu mmoja anataka kuhujumu hii haikubaliki.Na sisi kama chama cha wafugaji hatutakuwa tayari tunaomba msaidizi wa OCD aliyemuwakilisha atusaidie kumkata Chirstopher kwa kuwa ana nio ovu ya kuchafua ofisi ya DC.


Katika hatua nyingine Wambura alitumia fursa hiyo kuwaomba wafugaji hao kumpigia kura mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk, John Magufuli ili azidi kusimamia kikamlifu utekelezaji wa Ilani ya CCM ambayo imelenga kusaidia sekta ya mifugo katika nyanja mbalimbali.


"Niwaombe wafugaji wenzangu tucjague viongozi wanaotokana na CCM kuanzia ngazi ya diwani,mbunge na Rais ili washirikiane kwa pmoja kutatua kero mbalimbali za mafugaji".


Awali akizungumza  kwa niaba ya wafugaji hao Dan Kidaigure  amesema baada ya mifugo kuuzwa hawakupwa stakabadhi kama  mkuu wa wilaya  alivyoelekeza na hakuna ujenzi wowote uliofanyika.


"Baada ya mkuu wa wilaya kutuomba mwaka 2017 tulikubali kuchangisha mifugo yetu kwa ajili ya ujenzi wa shule,mifugo imeuzwa hatujapewa stakabadhi na hakuna ujenzi wowote uliofanyika tunaomba viongozi wa wafugaji Taifa mtusaidie ili waliouzwa mifugwe yetu wakamatwe na kuchukuliwa hatua".


Amesema  wananchi walichanga mifugo hiyo wakiamini kuwa mkuu huyo wa wilaya angesimamia zoezi hilo kikamilifu ili madarasa yajengwe  lakini ni zaidi ya miaka mitatu sasa bila wananchi kupata majibu  yeyote kutoka kwa mkuu huyo wa wilaya juu ya mifugo yao.


Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Pangani Zainabu alikiri kuhamasisha wananchi hao kuchanga mifugo hiyo plop ajili ya ujenzi wa madarasa mawili ya kidato cha tano na cha sita katika kata ya Bushiri.


"Baada ya kupata taarifa kuwa mifugo hiyo iliuzwa na fedha hazikuonekana ofisi yangu iliagiza ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) wilaya ya Pangani kwa hatua zaidi".

Share To:

msumbanews

Post A Comment: