Na Ferdinand Shayo ,Arusha.
Wanahabari nchini pamoja na Wahariri wa Vyombo vya Habari wamepatiwa mbinu za kupambana na ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji,ukekeketaji na ulawiti kwa kutumia kalamu zao kuibua vitendo hivyo ili viweze kutokomezwa kwa kushirikiana na serikali,pamoja na wadau mbalimbali.
Akizungumza katika Mafunzo ya kuwajengea uwezo Wahariri na Wanahabari liyondaliwa na Wizara ya Katiba na Sheria ,Msajili wa Mashirika yanayotoa msaada wa kisheria kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Felister Joseph amesema kuwa vitendo vingi vya ukatili vinavyofanyika haviripotiwi katika vyombo vya sheria kutokana na badhi ya wanajamii kushindwa kuvunja ukimya na kupaza sauti zao hivyo wanbahabari wanapaswa kuwa sauti yao.
Mtaalamu wa Masuala ya Jinsia na Ukatili Dr.Geofrey Chambua amesema kuwa wameamua kutoa mbinu kwa wanahabari juu ya namna ya kuripoti matukio ya ukatili bila kuwaumiza waathirika wa vitendo hivyo.
Kwa upande wao Wanahabari Janet Mushi na Godifrey Jackson wamesema kuwa mbinu walizopatiwa watazitumia kuhakikisha kuwa wanarioti vitendo hivyo kwa kufuata sheria,maadili na miioko .
Post A Comment: