Wachimbaji wadogo wa madini nchini wameshauriwa kutumia Ofisi za Tume ya Madini zilizopo Mikoani kwa lengo la kupatiwa elimu ya namna bora ya uchimbaji wa madini ambao utawasaidia kufanya shughuli za uchimbaji zenye tija.
Hayo yamebainishwa na Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Joseph Kumburu wakati alipotembelea banda la Tume ya Madini kwenye maonesho ya teknolojia na uwezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea Mkoani Geita.
Mhandisi Kumburu amesema kuwa, kwa sasa Serikali kupitia Tume ya Madini imeendelea kuweka mazingira salama ambayo lengo lake ni kumsaidia mchimbaji mdogo kwenye shughuli zake za kila siku.
Post A Comment: