Makamu Askofu Jimbo Katoliki la Singida, Padri Francis Lyimu akizungumza na Vijana (hawapo pichani) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Halmashauri ya Viwawa Taifa uliofanyika mkoani hapa leo.
Mratibu wa Vijana Wakatoliki Taifa, Padri Adolof Minga, akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Makamu Askofu Jimbo Katoliki la Singida, Padri Francis Lyimu na Damas Nderumaki, ambaye ni Meneja Mradi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Konrad Adenauer Stiftung (KAS), la Ujerumani lililofadhili mkutano huo.
Mratibu wa Mradi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) la Ujerumani, lililofadhili mkutano huo, Mary Tagalile, akizungumza katika mkutano huo.
Meneja wa Mradi wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) la Ujerumani, lililofadhili mkutano huo, Damas Nderumaki, akizungumza katika mkutano huo.
Mlezi wa Jimbo Katoliki Singida, Fr.Stefano Sinda, akizungumza.
Vijana washiriki wa mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Washiriki wakifuatilia mada.
Washiriki wakifuatilia mada.
Mada zikitolewa.
Washiriki wakifuatilia mada.
Wanafunzi wa Sekondary ya ST. Benard wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Vijana Jimbo la Geita, Mathayo Christian (kulia) akitoa shukurani kwaniaba ya wenzake baada Makamu Askofu Jimbo Katoliki la Singida, Padri Francis Lyimu kuzungumza nao.
Mwezeshaji katika mafunzo hayo Muhadhiri wa Chuo Kikuu cha SAUT cha jijini Mwanza, Pontian Ntui akitoa mada  kuhusu Uchumi wa Soko Jamii.
Umakini katika mkutano huo.
Viongozi meza kuu wakipiga makofi.
Makamu Askofu Jimbo Katoliki la Singida, Padri Francis Lyimu (katikati waliokaa) akiwa katika picha na Mratibu wa Vijana Wakatoliki Taifa, Padri Adolof Minga (wa tatu kushoto walio kaa) na Wawakilishi kutoka Shirika lisilokuwa la kiserikali la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) la Ujerumani pamoja na washiriki wote wa mkutano huo.
Makamu Askofu Jimbo Katoliki la Singida, Padri Francis Lyimu (katikati waliokaa) akiwa katika picha na Mratibu wa Vijana Wakatoliki Taifa, Padri Adolof Minga (wa tatu kushoto walio kaa) na Wawakilishi kutoka Shirika lisilokuwa la kiserikali la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) la Ujerumani pamoja na washiriki kutoka Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
Makamu Askofu Jimbo Katoliki la Singida, Padri Francis Lyimu (katikati waliokaa) akiwa katika picha na Mratibu wa Vijana Wakatoliki Taifa, Padri Adolof Minga (wa tatu kushoto walio kaa) na Wawakilishi kutoka Shirika lisilokuwa la kiserikali la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) la Ujerumani pamoja na washiriki kutoka Jimbo Kuu la Dodoma.
Makamu Askofu Jimbo Katoliki la Singida, Padri Francis Lyimu (katikati waliokaa) akiwa katika picha na Mratibu wa Vijana Wakatoliki Taifa, Padri Adolof Minga (wa tatu kushoto walio kaa) na Wawakilishi kutoka Shirika lisilokuwa la kiserikali la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) la Ujerumani pamoja na washiriki kutoka Jimbo Kuu la Tabora.
Makamu Askofu Jimbo Katoliki la Singida, Padri Francis Lyimu (katikati waliokaa) akiwa katika picha na Mratibu wa Vijana Wakatoliki Taifa, Padri Adolof Minga (wa tatu kushoto walio kaa) na Wawakilishi kutoka Shirika lisilokuwa la kiserikali la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) la Ujerumani pamoja na washiriki kutoka Jimbo Kuu la Mwanza.
Makamu Askofu Jimbo Katoliki la Singida, Padri Francis Lyimu (katikati waliokaa) akiwa katika picha na Mratibu wa Vijana Wakatoliki Taifa, Padri Adolof Minga (wa tatu kushoto walio kaa) na Wawakilishi kutoka Shirika lisilokuwa la kiserikali la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) la Ujerumani pamoja na washiriki kutoka Jimbo Kuu la Mbeya.
Makamu Askofu Jimbo Katoliki la Singida, Padri Francis Lyimu (katikati waliokaa) akiwa katika picha na Mratibu wa Vijana Wakatoliki Taifa, Padri Adolof Minga (wa tatu kushoto walio kaa) na Wawakilishi kutoka  Shirika lisilokuwa la kiserikali la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) la Ujerumani pamoja na washiriki kutoka Jimbo Kuu la Songea.
Makamu Askofu Jimbo Katoliki la Singida, Padri Francis Lyimu (katikati waliokaa) akiwa katika picha na Mratibu wa Vijana Wakatoliki Taifa, Padri Adolof Minga (wa tatu kushoto walio kaa) na Wawakilishi kutoka  Shirika lisilokuwa la kiserikali la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) la Ujerumani pamoja na washiriki kutoka Jimbo Kuu la Arusha.
Makamu Askofu Jimbo Katoliki la Singida, Padri Francis Lyimu (katikati waliokaa) akiwa katika picha na Mratibu wa Vijana Wakatoliki Taifa, Padri Adolof Minga (wa tatu kushoto walio kaa) na Wawakilishi kutoka Shirika lisilokuwa la kiserikali la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) la Ujerumani pamoja na Walezi wa Vijana kutoka Majimboni. 


Na Dotto Mwaibale, Singida.


VIJANA nchini wametakiwa kuifanyia kazi elimu waliyoipata kwa ajili ya kuinua uchumi wao binafsi na Taifa kupitia Uchumi wa Soko Jamii.

Wito huo umetolewa na Makamu Askofu Jimbo Katoliki la Singida, Padri Francis Lyimu wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Halmashauri ya Viwawa Taifa uliofanyika mkoani hapa leo.

Mkutano huo uliofadhiliwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) la Ujerumani ulienda sambamba na kuwajengea uwezo viongozi wa vijana taifa katika kushiriki barabara masuala ya utawala hususani katika uchumi wa soko jamii.

Akizungumza na vijana waliochaguliwa kuwa viongozi wa vijana katika majimbo yao amewataka kuwa na utume mzuri kwani utume wa vijana ni nguzo ya Kanisa hivyo kwa kuchaguliwa wao wanatakiwa kuwachota vijana ambao bado wapo pembeni na kuibua vipaji  vyao.

Lyimu aliwataka vijana kushirikiana na kanisa katika utume wao na waufurahie ujana wao kwa manufaa ya nchi na kanisa kwa ujumla na hata wakiambiwa wamekosea wawe na nafasi ya kujisahihisha na kusimama tena.

" Kijana lazima aonekane katika mtazamo mpya ambao  hauondoi tunu zao lakini unaleta mabadiliko katika mtazamo wao wao na hasa kuwa na dira ya kimaendeleo kwa utendaji wenye tija." alisema Lyimu.

Alisema Mungu alipomuumba mwanadamu alimwambia autawale ulimwengu na viumbe vilivyomo na kufanya kazi.

Lyimu aliwataka vijana katika utendaji kazi wao ndani ya nchi na kanisa kuacha alama badala ya kukaa vijiweni kwa kupiga stori.

Aidha Lyimu aliwataka vijana kufanya lilelinalo wezekana kwa wakati na si kusubiri lifanyike baadae na lifanyike kwa malengo.

" Vijana ondokeni na neno 'siwezi' na haiwezekani' kitu gani kisichowezekana kama vijana mnatakiwa kusimama na sio kusalimu amri ya kushindwa pambaneni mpaka kieleweke." alisema Lyimu.

Aliwataka vijana hao kumpenda Mungu na kumtunikia kwa kuzingatia misingi yote ya imani ya Kanisa Katoliki.

Lyimu alisema ni lazima vijana kujishughulisha kwa kujiajiri na kuwa haiwezekani nuhitimu wa darasa la saba aendeshe maisha yake kwa kujiajiri na muhitimu wa chuo kikuu aendelee kulia na ajira kwa kuomba hata vocha kwa wazazi wao.

Aliwataka vijana kushiriki katika shughuli za maendeleo na hata siasa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu na kanisa.

Mwezeshaji katika mafunzo hayo Muhadhiri wa Chuo Kikuu cha SAUT cha jijini Mwanza, Pontian Ntui akitoa mada  kuhusu Uchumi wa Soko Jamii aliwataka vijana hao kuwa wabunifu na kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ya ufugaji badala ya kutegemea kuajiriwa.

Share To:

Post A Comment: