Leo tarehe 27 Septemba, 2020 Tume ya Madini imepata kikombe cha ushindi mara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kwenye Kundi la Taasisi Wezeshi za Serikali Sekta ya Madini katika Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yaliyohitimishwa katika Uwanja wa Kituo cha Uwekezaji Bombambili Geita Majini .
Akizungumza mara baada ya Tume ya Madini kukabidhiwa kikombe hicho Katibu Mtendaji wake, Profesa Shukrani Manya amesema kuwa siri ni ubunifu na uzalendo wa wataalam kwenye utoaji wa elimu katika maonesho hayo.
Wakati huohuo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu –Uwekezaji aliyekuwa mgeni rasmi kwenye ufungaji wa maonesho hayo, Angellah Kairuki ametembelea banda la Tume ya Madini na kupongeza kwa kazi kubwa hususan kwenye ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali.
Zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali
Post A Comment: