Aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Jonathan Shana amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.
Taarifa ya kifo chake imethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Hospitali ya Taifa Muhimbili Aminiel Aligaesha na kusema kuwa marehemu alikaa hospitali kwa siku 21 na kati ya hizo alikaa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU), kwa siku tatu.
Kamanda Shana aliwahi kuwa Kamanda wa Polisi (RPC) katika Mkoa ya Pwani, Mwanza na Arusha.
ACP Jonathan Shana amefariki akiwa Afisa Mnadhimu Namba Moja katika Chuo cha Polisi (CCP) mkoani Moshi.
Post A Comment: