Naibu Katibu mkuu Wizara ya elim Sayansi na Teknolojia Prof James Mdoe ameitaka Taasisi ya elim ya Watu ya wazima (TEWW) kuwa wabunifu katika kutoa mawazo yatakayolenga kuanzisha mikakati bora itakayowawezesha kukabiliana na changamoto wanazokutana nazo.

Rai hiyo ameitoa mapema leo jijini Dar es Salaam leo wakati wa maadhimisho ya kilele Cha Juma la elimu ya watu wazima sambamba  na kuzindua mkakati wa kitaifa wa kukuza na kuendeleza kisomo na elimu kwa Umma nchini Tanzania.

Aidha ameitaka Taasisi hiyo kuusimamia kikamilifu mkakati huo kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ili uweze kua endelevu na kutoa matokeo chanya katika jamii katika kukuza kujua kusoma, kuandika na kuhesabu.

"Naomba niwapongeza sana TEWW mumefanya kazi kubwa kuzindua mpango mkakati huu wa miaka mitano (2020/2021_2024/2025) lakini nataka niwambie kitu, kuzindua mkakati ni kitu kimoja na kutekeleza ni kitu chengine, naomba mujiongeze musiwe na mawazo ya zamani"amesema Prof Mdoe.

Amesema kuwa, anaimani mkakati huo utakua dira kwa wadau wote katika kukuza na kuendeleza kisomo na elimu kwa umma nchini,huku akiwaomba wadau hao kutumia mpango mkakati huo katika kuanzisha na kuyaendeleza madarasa ya kisomo katika maeneo yao.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya elimu ya watu wazima Dkt Michael Ng'umbi amesema kuwa,lengo la kuzindua mkakati huo ni kupunguza idadi ya vijana na watu wazima na watu wazima wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) ambapo wanakadiriwa kuwa mill 5.5 kulingana na sensa ya 2014.

Amesema kuwa, mkakati huo pia umelenga kuboresha kukuza na kuendeleza kisomo na elim kwa umma katika maeneo nane ikiwemo kujenga uwezo wa wawezeshaji na waratibu wa program za EWW na elimu kwa umma nchini.

"Pia tutaboresha kuweka viwango vya sifa,kuandaa zana bora za kujifundishia na kujifunzia program za EWW,kukuza shughuli za utafiti,ubunifu na ugunduzi katika masuala ya EWW, kuimarisha mifumo ukusanyaji na utunzaji wa takwim za EWW pamoja na kubuni na kuendeleza mipango ya EWW"amesema Dkt.Ng'umbi.

Naye, mkuu wa Kitengo Cha elimu UNESCO Faith Shayo akitoa hutuba ya Mkurugenzi wa Shirika hilo, Tirso Dos Santos amesema kuwa,kusoma na kuandika ni lengo la nne la Maendeleo endelevu ambayo inayojumuisha kutoa elimu bora na kukuza maisha ya binaadam.

Aidha amesema kuwa,lengo la Maendeleo endelevu namba 4.6  ifikapo 203O vijana wote na idadi ya watu wazima wanaume na wanawake wawe wamefanikiwa kusoma na kuhesabu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: