Spika wa Bunge Job Ndugai (katikati) akikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Manyoni mkoani Singida jana. Kutoka kulia ni Mkuu wa Takukuru Wilaya ya Manyoni,  Jarome Mpanda, Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa, Sabina Seja, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kepteni Mstaafu George Mkuchika, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Magwisa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Manyoni Magharibi, Yahaya Masere.
Spika wa Bunge Job Ndugai (katikati) akipiga makofi baada ya kuweka jiwe la msibgi la  jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kepteni Mstaafu George Mkuchika, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa, Sabina Seja, akizungumza kwenye hafla hiyo.
 Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Rahabu Magwisa, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Spika wa Bunge Job Ndugai, akisalimia na Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Singida, Adili Elinipenda.




Muonekano wa jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.
Baadhi ya Watumishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wakiwa kwenye hafla ya ufunguzi wa jengo hilo.
Wananchi wakiwa kwenye hafla ya ufunguzi wa jengo hilo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondary ya Mlewa wakitoa burudani.
Wasanii wa Kundi la Terminator wakitoa burudani.


Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Wimbo wa Taifa ukiimbwa.
Sheikh wa Wilaya ya Manyoni, Hassani Ndagowe,  akiomba dua kabla ya kuanza hafla hiyo.
Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Rift Valley Manyoni, John Lupaa, akiomba kabla ya kuanza hafla hiyo.
Kwaya ya Takukuru kutoka Dodoma ikitoa burudani.
Ufunguzi wa Jengo hilo ukiendelea.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondary ya Manyoni wakiwa kwenye hafla ya ufunguzi wa jengo hilo.
Wagombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Yahaya Masere (kulia) wa Jimbo la Manyoni Magharibi na Pius Chaya wa Jimbo la Manyoni Mashariki wakiteta jambo katika hafla hiyo.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Manyoni wakiwa kwenye hafla hiyo.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.


Na Dotto Mwaibale, Manyoni.

SPIKA wa Bunge Job Ndugai ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuhakikisha Watanzania hawarubuniwi katika kipindi hiki cha uchaguzi Mkuu na  wanatumia vizuri utashi wao wa kisiasa kuchagua viongozi bora wanaowataka.

Ndugai ambaye alikuwa mgeni rasmi alitoa ombi hilo jana wakati akifungua jengo la Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Manyoni mkoani Singida ambalo ni moja ya majengo kati ya saba yaliyojengwa na Serikali katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2017/2018 kwa jumla ya sh.bilioni 1.

"Sote tunatambua kuwa Oktoba 28 mwaka huu Taifa letu litaendesha Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na Madiwani Takukuru mnalojukumu zito katika kuhakikisha Watanzania hawarubuniwi ili watumie vizuri utashi wao wa kisiasa kuchagua viongozi bora watakaoshirikiana nao katika kujiletea maendeleo" alisema Ndugai.

Katika hatua nyingine Ndugai aliwataka watumishi wa Takukuru kuwa wacha Mungu na watende kazi zao kwa haki pasipo kumuone mtu na wawekeze zaidi kutoa elimu kwa watu ili waweze kujiepusha na vitendo vya rushwa.

Ndugai pia aliwaomba Takukuru kumaliza kesi haraka na kueleza kuwa zinapochukua muda mrefu zina wasababishia watuhumiwa kuwa na  msongo wa mawazo.

Aidha Ndugai aliiomba jamii kushirikiana na Takukuru na kuacha tabia ya fitina ya kuwazushia watu kesi za uongo na kueleza kuwa ni jambo baya katika  taifa letu.

Ndugai alitumia nafasi hiyo kumpongeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora pamoja na Mkurugenzi Mkuu Takukuru kwa kusimamia vema mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi ndani na nje ya Serikali.

Alisema hatua hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kudhibiti matumizi ya hovyo ya fedha za umma sambamba na kuongeza usimamizi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kuziba mianya ya ukwepaji kodi na Serikali kufanikiwa kutekeleza miradi mingi hadi vijijini ikiwemo ujenzi wa ofisi na nyumba za Takukuru.

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kepteni Mstaafu George Mkuchika alisema anaungana na Rais Dkt.John Magufuli kwa kuipongeza Takukuru kwa kazi nzuri wanaoifanya katika kuzuia na kupambana na watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa hapa nchini.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uzuiaji Rushwa Sabina Seja, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru alisema wanamshukuru Rais Magufuli kwa kuiwezesha Takukuru kujenga jengo hilo pamoja na kupata vitendea kazi, rasilimali fedha na watu msaada ambao wamekuwa wakiupata mara kwa mara.

"Serikali haina fursa ya kukubaliana na vitendo vyote vya ubadhilifu wa mali ya umma pamoja na rushwa katika kuiimarisha Takukuru kiutendaji kazi" alisema Seja.

Alisema watumishi wa  Takukuru kwa ujumla wao wamefarijika sana na dhamira ya Rais Dkt.John Magufuli ya kuimarisha utendaji wao wa kazi, ujenzi wa majengo  hayo ya  ofisi yaliyojengwa kwa wakati mmoja katika wilaya saba za Manyoni mkoani Singida, Masasi mkoani Mtwara, Namtumbo mkoani Ruvuma, Ruangwa mkoani Lindi, Mpwapwa mkoani Dodoma, Ngorongoro mkoani Arusha  na jengo la ofisi za Intelijensia lililopo jijini Dodoma. 

Share To:

Post A Comment: