Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dk.John Jingu, akisisitiza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa miongozo saba ya huduma ya ustawi wa jamii na muundo mmoja wa maendeleo ya utumishi wa kada ya ustawi wa jamii iliyofanyika jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dk.John Jingu,(hayupo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa miongozo saba ya huduma ya ustawi wa jamii na muundo mmoja wa maendeleo ya utumishi wa kada ya ustawi wa jamii iliyofanyika jijini Dodoma.

Kamishna wa Ustawi wa Jamii Dkt. Naftali Ng’ondi,akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa miongozo saba ya huduma ya ustawi wa jamii na muundo mmoja wa maendeleo ya utumishi wa kada ya ustawi wa jamii iliyofanyika jijini Dodoma.

Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), Dk.Qasim Sufi,akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa miongozo saba ya huduma ya ustawi wa jamii na muundo mmoja wa maendeleo ya utumishi wa kada ya ustawi wa jamii iliyofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afya, Ustawi wa jamii na Lishe kutoka TAMISEMI, Rashid Maftaa,akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa miongozo saba ya huduma ya ustawi wa jamii na muundo mmoja wa maendeleo ya utumishi wa kada ya ustawi wa jamii iliyofanyika jijini Dodoma.

Kamishna Msaidizi Idara ya Ustawi wa Jamii Bi.Mwanaisha Moyo akitoa taarifa wakati wa hafla ya uzinduzi wa miongozo saba ya huduma ya ustawi wa jamii na muundo mmoja wa maendeleo ya utumishi wa kada ya ustawi wa jamii iliyofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dk.John Jingu, (wa pili kutoka kulia) akizindua miongozo saba ya huduma ya ustawi wa jamii na muundo mmoja wa maendeleo ya utumishi wa kada ya ustawi wa jamii iliyofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dk.John Jingu, akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua miongozo saba ya huduma ya ustawi wa jamii na muundo mmoja wa maendeleo ya utumishi wa kada ya ustawi wa jamii iliyofanyika jijini Dodoma.

..................................................................

Na. Alex Sonna, Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dk.John Jingu, amezindua miongozo saba ya huduma ya ustawi wa jamii na muundo mmoja wa maendeleo ya utumishi wa kada ya ustawi wa jamii ili kuwa na msingi wa taifa katika huduma hiyo.

Dkt.Jingu amezindua miongozo hiyo jijini Dodoma iliyohudhuriwa na wizara mbalimbali pamoja na wadau

 

Dkt. Jingu amesema kuwa miongozo hiyo imetengenezwa baada ya kufanya utafiti na kutumia mbinu mbalimbali za kisayansi ili kupata vitu vitakavyosaidia kuwa na miongozo bora.

Aidha Dkt. Jingu amesema kuwa katika miongozo hiyo saba kuna wa uanzishaji wa nyumba salama kwa ajili ya wahanga wa ukatili na usafirishaji wa binadamu.

Lakini pia Dkt. Jingu amesema kuna mwongozo wa wawakilishi wa watoto mahakamani unaoweka utaratibu wa upatikanaji wawakilishi na kuainisha majukumu yao katika kuwasaidia watoto wakati wa uendeshaji mashauri mahakamani

“Mingine ni wa kuwaunganisha watoto na familia zao, utambuzi wa huduma kwa watoto walio katika mazingira hatarishi na mwongozo wa majukumu ya maafisa ustawi wa jamii katika Mamlaka za Serikali za Mitaa,”ameeleza Dkt.Jingu.

Dk.Jingu amesisitiza kuwa muongozo huo unalenga kubainisha kwa kina majukumu hasa ya maafisa ustawi wa jamii ili kuondoa mkanganyiko uliookuwepo wa kufanya kazi zilizopaswa kufanya na Ofisa Maendeleo ya jamii au mtu mwingine.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), Dk.Qasim Sufi, ameeleza kuwa duniani kuna wahanga takribani Milioni 20.9 wanaolazimishwa kufanya kazi, usafirishaji haramu wa binadamu jambo ambalo linapaswa kukomeshwa

Huku Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afya, Ustawi wa jamii na Lishe kutoka TAMISEMI, Rashid Maftaa, ameweka wazi kuwa ofisi hiyo imejipanga kuhakikisha miongozo hiyo inatekelezwa ipasavyo ili kuwa na huduma bora za ustawi wa jamii katika msingi wa Taifa .

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: