Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya Wananchi (hawapo pichani) katika  mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Bombadia mjini Singida jana.

Umati wa Wananchi wa Mkoa wa Singida wakisikiliza hutuba ya mgombea huyo wa Urais
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iramba Mashariki, Francis Isack akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini, Ramadhani Ighondo,  akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki, Yahaya Masere akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu,  akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Aysharose Mattembe,akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Tatu Ntandu,akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Singida, Martha Gwau,akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba, akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mussa Sima, akijinadi kwa Wananchi mbele ya Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli.


Na Dotto Mwaibale, Singida

SERIKALI imetumia Sh. Bilioni 470.4 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Singida.

Hayo  yalisemwa na  Mgombea Urais wa Chama  cha  Mapinduzi (CCM)   Rais  Dkt. John Magufuli wakati akiwahutumia maelufu ya wanannchi katika mkutano wake wa pili wa kampeni wa kuomba ridhaa ya kuongoza nchi kwa awamu ya pili uliofanyika viwanja vya Bombadia mjini hapa jana.

Magufuli alisema katika kipindi cha miaka mitano Serikali imefanikiwa kujenga vituo vya afya vilivyowezesha akinama 730 kufanyiwa upasuaji hivyo kuokoa maisha yao na watoto wao.

Alisema mbali ya vituo hivyo vya afya serikali imejenga Hospitali tatu za wilaya  katika Wilaya za Mkalama, Ikungi na Singida.

" Ndani ya  kipindi hicho viwanda zaidi ya 8,500 vimejengwa katika mkoa huu huku tukizalisha ajira milioni sita  na kama mtanipa ridhaa ya kuongoza nchi kwa mara nyingine tena tutazalisha ajira milioni 8." alisema Magufuli huku akishangiliwa.

Aidha Magufuli alisema Sh. bilioni 52.6 zimetumika kujenga miundombinu ya shule yakiwemo madarasa, maabara na miundombinu mingine huku Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida  Mandewa ikiwa katika hatua za mwisho kukamilika na hiyo ni moja ya hatua ya kuboresha sekta ya afya.

Mgombea huyo wa Urais alisema kulikuwa na vijiji 2018 tu vilivyokuwa vimefikishiwa  umeme mwaka 2015 lakini katika miaka mitano ya uongozi wake vijiji 9570 vimefikiwa kati ya vijiji 12280 nchi nzima huku sh. bilioni 310 zikitumika kujenga miundombinu wezeshi na sh. bilioni 27.2 zikitumika kutekeleza miradi ya maji ipatayo 66.

Akiongelea uandikishaji wanafunzi umeongezeka kutoka milioni 1 hadi milioni 1.6 baada ya kuanza kwa mpango wa elimu bure.

Magufuli aliongeza kuwa katika kipindi hicho jumla ya sh. bilioni 17 zimetumika kujenga barabara za Singida mjini na kuziwekea taa huku ujenzi wa barabara ya Chaya Singida hadi Tabora ikibakia kilometa tu 20 kukamilika.

Alisema viituo vya afya 487 vimejengwa Tanzania nzima na bwawa kubwa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere litakalozalisha megawati 2,115.

Alisema vijiji 9,570 vimefikiwa na nishati ya umeme ikilinganishwa na vijiji 2,018 vilivyokuwa na umeme mwaka 2015.
Alisena katika kipindi hicho bajeti ya Wizara ya Afya imeongezwa kutoka sh. bilioni 30 hadi bilioni 270.

" Niko hapa kwa unyenyekevu mkubwa kuomba kura za vyama vyote kwa sababu maendeleo hayana chama" alisema Magufuli.

Magufuli alisema katika kipindi hicho katika Mkoa wa Singida visima vinne virefu vimechimbwa ili kuongeza upatikanaji wa maji ambapo sh. bilioni 66 zimetumika kutekeleza miradi ya maji na kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji kutoka asilimia 41 hadi 54.

Alisema mbali ya kutekeleza miradi hiyo ya maji shule kongwe ikiwemo Mwenge Sekondari zimekarabatiwa ikiwa ni moja ya hatua za kuboresha sekta ya elimu.

Alisema ukusanyaji wa mapato umeongezeka kutoka wastani wa sh. bilioni 850 hadi kufikia zaidi ya sh.Trilioni 1.5 huku Tozo 114 zikifutwa katika sekta ya kilimo na wafanyabiashara ndogondogo wakifutiwa kodi 54.

Alisema Serikali imeweza  kukusanya   sh Ttrioni1.5-1.9 kwa  mwezi  ukilinganisha na Bilioni  850 zilizokuwa zikiikusanywa hapo awali.
Akiendelea kuongelea mafanikio ya Seikali kwa kipindi hicho cha miaka mitano alisema kwa mujibu wa ripoti ya  "Global Peace Index" Tanzania imekuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki, ya 6 Afrika na 52  duniani kwa amani.

Magufuli aliongeza kueleza kuwa ndani ya miaka hiyo mitano mitandao ya simu imeimarika nchi nzima huku waki jenga ukuta wa kilometa  25 eneo la Mererani ambao umesaidia  kudhibiti  wizi wa madini ya Tanzanite na upotevu wa mapato ya nchi.

Mgombea huyo alimaliza hutuba yake kwa kuwanadi wagombea wote wa nafasi ya ubunge na udiwani wa chama hicho pamoja na kumshukuru Mungu kwa kutuepusha na janga LA Corona kutokana  na maombi tuliyofanya kama taifa na kuwa hiyo imetoa somo kubwa kwa mataifa mengi duniani kuwa Mungu anaweza.
Share To:

Post A Comment: