Na Mwandishi Wetu – ORCI

Serikali imesimika mashine kisasa ya mammography ambayo ni maalum kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa saratani ya matiti, katika Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI).

Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa ORCI, Dk. Crispin Kahesa amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari mapema hii leo na kusisitiza kwamba mashine hiyo ipo tayari kutumika wakati wowote kuanzia sasa.

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha inaboresha huduma za uchunguzi wa saratani hiyo ambayo sasa takwimu za taasisi hiyo zinaonesha imeanza kugundulika pia kwa wanawake wenye umri mdogo.

“Ina uwezo mkubwa wa kuwezesha wataalamu kufanya uchunguzi, tunapoelekea Oktoba ambao ni mwezi wa uhamasishaji, uelimishaji kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu saratani ya matiti, pia kutafanya uchunguzi na matibabu kwa watakaogundulika, tutaanza rasmi kuitumia mashine hii ya kisasa,” amesisitiza.

Juzi, Dk. kahesa alinukuliwa akisema kwamba saratani hiyo bado ni tishio nchini na wastani wa umri wa wanawake wanaokutwa nayo umeshuka kutoka miaka 64 mwaka 2008/09 hadi miaka 56 mwaka 2019.

Mkurugenzi Mtendaji wa ORCI, Dk. Julius Mwaiselage amebainisha mashine hiyo imenunuliwa kutoka Korea Kusini kwa kiasi cha Sh. Mil 189 kupitia Bohari Kuu ya Dawa (MSD).


 *MWISHO*
Share To:

msumbanews

Post A Comment: