Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya ametembelea mabanda ya Wizara ya Madini kwenye Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea katika Uwanja wa Kituo cha Uwekezaji Bombambili Geita Majini .
Mara baada ya kutembelea Banda la Tume ya Madini kwenye maonesho hayo, amepongeza kazi nzuri iliyofanywa na wataalam wa Tume na kuwataka kuendelea kuelimisha umma hasa wachimbaji wadogo kuhusu Sheria ya Madini na kanuni zake, usalama wa afya na mazingira wanapoendesha shughuli za uchimbaji wa madini na biashara ya madini.
Aidha ameelekeza elimu kuhusu ushirikishwaji wa watanzania kwenye Sekta ya Madini kuendelea kutolewa ili kutoa fursa kwa wananchi wengi kushiriki kwenye sekta ya Madini.
Zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali
Post A Comment: