Na John Walter-Manyara
Polisi mkoani Manyara wameripoti kuwatia mikononi watuhumiwa 6 wa madawa ya kulevya aina ya Bangi misokoto 36 na wengine 11 wakiwa na Pombe haramu Gongo lita 139.5 na mmoja akiwa na mitambo ya kuchemsha Pombe hiyo.
Kamanda wa
Polisi mkoa wa Manyara Paul Kasabago amearifu
kwamba operesheni ilitekelezwa kuanzia Agosti
20,2020 hadi Septemba 4,2020 kwa lengo
la kuwakomboa wanannchi katika utumiaji
wa madawa hayo.
Aidha Kasabago
amesema katika Operesheni hiyo wamewakamata watu 9 wakiwa na mali ambazo zinadhaniwa kuwa ni
za wizi ambazo ni Cherehani moja aina ya Butterfly, Jiko la gesi moja aina ya
Opex ambazo zote zina thamani ya shilingi 195,000 pamoja na Generator aina ya
Honda H2000 na Speaker moja zenye thamani ya shilingi 2,500,000 moja ambazo ni
mali ya Kanisa la Tanzania Tanzania Assemblies of God (TAG) lililopo wilaya ya Hanang’.
Amesema
katika operesheni hiyo jumla ya watuhumiwa 25 walikamatwa na wote wamefikiswa
mahakamani kujibu tuhuma mbalimbali zinazowakabili na kesi zao zipo katika hatua za kutajwa na
zingine kusikilizwa.
Kamada Kasabago amewataka
wale wanaofanya biashara haramu kuacha mara moja na kutafuta biashara zingine
zitakazoweza kuwaingizia kipato kwa njia halali.
Post A Comment: