Na Woinde Shizza , ARUSHA
Jeshi la polisi mkoani Arusha linawashikilia watuhumiwa watatu wanaohusika na tukio la kuchoma Moto ofisi za Chama Cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) tukio lililotokea agost 14 majira ya Saa tatu usiku katika kata ya Kimandolu ,Tarafa ya Suye iliopo ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Arusha ACP Salim Hamduni alisema kuwa watuhumiwa hao waliokamatwa walisababisha uharibifu wa Mali zenye thamani ya shilingi 5,680,520 baada ya kufanyiwa tathmini.
Alisema kuwa Mara baada ya kufanya uchunguzi wa kina uliofanyika awaliwabaini na kuwakamata watu wote waliohusika katika tukio hilo Ambapo agost 19 mlinzi wa ofisi hiyo ya CHADEMA aliejulikana kwa jina la Deogratius Malya,nawaliendelea na uchunguzi uliendelea Ambapo agost 26,28 watuhumiwa wengine wawili walikamatwa ambao aliwataka kwa jina Leonard Ntukula (65) mngoni dereva wa chadema na mkazi wa Tabata jijini Dar es salaam pamoja Prosper Makonya( 55) mjita ambaye ni afisa mhamasishaji wa CHADEMA makao makuu na mkazi wa makongo jijini Dar es salaam.
Aidha alibainisha kuwa baada ya kukamilisha upelelezi jalada la kesi limeelekwa ofisi ya taifa ya mashtaka kwa ajili ya kulisoma na kulitolea Maamuzi au maelezo ya kisheria ya kisheria ikiwa ni pamoja na kuandaa hati ya mashtaka ,na watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili baada ya kukamilika kwa taratibu za kisheria.
Hamduni alitoa onyo kwa baadhi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu waepuke kupanga na kufanya matukio yeyote ya kiuhalifu hasa katika kipindi hiki Cha uchaguzi kwani polisi wapo imara na wanafatilia yeyote atakayebainisha kupanga na kufanya uhalifu atakamatwa bila kujali anatokea kundi gani
"Pia niwaombe wananchi wa Arusha kuendelea kutoa taarifa kwa polisi na vyombo vingine vya dola ili Kuhakikisha mkoa wetu unaendelea kuwa salama muda wote wa uchaguzi na hata baada hapo"alisema Hamduni
Aidha alitoa wito kwa wanasiasa wanaogombania nafasi mbalimbali Ndani ya mkoa wa Arusha kufanya kampeni za kistaarabu kuepuka na kutoa lugha au kauli za kuashiria uvunnjifu wa amani na kufanya vitendo ambavyo vipo kinyume Cha Sheria.
Post A Comment: