Mgombea Ubunge jimbo la Arumeru Mashariki kupitia chama cha Nccr Mageuzi Evva kaaya amezindua kampeni zake kwa kishindo huku akimwaga Sera ya kusaidia wanawake watoto kupata haki sawa na kuimarisha  Afya kwa kila kata kupata zahanati

Akizungumza katika viwanja vya shule ya msingi Nkoanrua  Evva amesema kwamba kikubwa kilicho msukuma kugombea ubunge jimbo la Arumeru Mashariki ni kusaidia wananchi kupata maendeleo katika kipindi cha miaka mitano cha utumishi wake


Amesema jimbo hilo kwa muda limekosa mwakilishi mwenye uchungu wa maendeleo na wengine waliopota kuwa wabunge wamekuwa wakijinufaisha wenyewe na sio kuleta maendeleo

Aidha amesema endapo atachaguliwa atakikisha anafanya kazi ya uwakilishi ya kuleta maendeleo kwa wananchi baada ya kuwatumikia vyema kwa mika mitano akiwa Diwani wa ambapo ameleta maendeleo makubwa katika kata Nkoanrua

Naye msimamizi wa uchaguzi kupitia Nccr Mageuzi Taifa  Atonny Komu ambaye pia ni Mgombea Ubunge jimbo la Moshi vijijini amesema chama chao kimemsimamisha Evva kwani historia  ya jimbo hilo lilisha ongozwa na chama hicho Mwakab 1995 hivyo wananchi wana imani kubwa na Nccr Mageuzi

Amesema watajikita kutatua changamoto za wananchi katika majimbo yote walio simamisha wagombea nchi nzima kwani sera yao ni kutumikia wananchi na kupata haki sawa na maendeleo.

Kwa upande wao wananchi waliojitokeza kusikiliza Sera katika ufunguzi wa kampeni hizo wamesema kwamba wamekuwa na utuba za mgombea na wana imani endapo watamchagua wqtakua wamemoata mwakilishi sahihi wa kutatua matatizo yao
Share To:

msumbanews

Post A Comment: