Na John Walter-Babati


Mwanaume mmoja aliejulikana kwa jina Ali Salimu (46) mkazi wa mtaa wa Maisaka B Kata ya Maisaka mjini Babati  amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani.

Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Paul Kasabago ambapo ameeleza kuwa mtu huyo alikuwa akining’inia kwenye kenchi la nyumba ndani ya chumba cha kulala cha Baba yake aitwaye Salimu Hassan.

Amesema  chanzo cha Mtu huyo kujinyonga  bado hakijafahamika na kwamba hakuacha ujumbe wowote na hapakuwa na ugomvi wowote wa kifamilia au na mtu yeyote.

Kamanda Kasabago amesema uchunguzi unafanyika ili kubaini mtu au watu waliohusika na tukio hilo ili waweze kuchukuliwa hatua kwa Mujibu wa sheria.

 

 

Share To:

Post A Comment: