Na Woinde Shizza, Arusha
Mgombea ubunge Jimbo la Arusha mjini kupitia Chama Cha ADA TADEA Zuber Mwinyi amehaidi kuchukuwa Jimbo la Arusha mjini na kuwamwaga wagombea wengine ambao Ni Godbless Lema mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA Pamoja na Mgombea ubunge wa CCM katika Jimbo hilo ambaye ni Mrisho Gambo kwani yeye Ni kiongozi makini aliejipanga kuleta Maendeleo Ndani ya Jimbo hilo
Aliyasema hayo Jana wakati wa uzinduzi wa kampeni wa Chama hicho ambao uliofanyika katika viwanja vya standi kubwa ya mabasi ya mkoani Arusha ambapo Alisema kuwa yeye ni mgombea tofauti na wengine kwani yeye hagawi fedha kwa wananchi ili wamchague bali anawaambia wananchi nini atawafanyia pindi wanapomchagua.
Alisema kuwa iwapo wananchi wa Jimbo la Arusha mjini wakimchagua atahakikisha anasimamia rasilimali zote za Jimbo la Arusha mjini ili ziweze kuwanufaisha wananchi wote .
Aidha Alisema kuwa atahakikisha wafanyabiashara wote wanakuwa marafiki na TRA kwa kuhakikisha wanakadiriwa Kodi zenye viwango vinavyoendana na biashara zao ,ambapo Alisema kuwa atatengeneza mpango maalum wa kurudisha biashara zote zilizofugwa na hatakaa kila Mara na wafanyabiashara ili kupata njia rahisi na nzuri za kuendeleza biashara zao
Kwa upande wa bodaboda Alisema kuwa anampango wa kutengeneza mpango mkakati wa Vijana wa usafirishaji ili waweze kupata mikopo ya bajaji na Toyo kwa Bei nafuu na bila riba .
Aliongeza kuwa atahakikisha wamama wote wajawazito wanapoenda kujifungua hawalipishwi kitu chochote kile pale wanapoingia hospitali Hadi pale wanaporuhusiwa kurudi majumbani mwao.
"Kwakuwa elimu Ni kila kitu nitaweka kitengo maalum Cha kusaidia mikopo ya wanafunzi iweze kupatikana kwa wakati Ndani ya Jimbo letu na kwakuwa elimu ni bure nitahakikisha kila mtoto anaeanza shule mzazi wake hawalipishwi mchango wowote ule na nitaakikisha madarasa yanajengwa ya kutosha na madawati yanakuwa ya kutosha kulingana na idadi ya wanafunzi"Alisema Zuber
Aliwataka wananchi kuchagua viongozi watakao badilisha maisha yao na wasichague viongozi kwa kuhamasishwa na vyama.
Post A Comment: