Katibu Mwenezi wa  CCM Mkoa wa Singida,Ahmed Kaburu,akitoa taarifa kwa waandishi habari (hawapo pichani) juu ya ziara ya Mgombea Mwenza nafasi ya Rais kupitia CCM na Makamu wa Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan atakayoifanya kuanzia kesho.


Na Waandishi Wetu, Singinda.

MGOMBEA Mwenza nafasi ya Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama, Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya kampeni mkoani Singida kuanzia kesho za kumuombea kura mgombea Urais wa chama hicho Dkt. John Magufuli, wabunge na madiwani. 

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Katibu Mwenezi CCM Mkoa wa Singida, Ahmed Kaburu, alisema mgombe mwenza huyo kampeni hiyo kwa kufanya mikutano ya hadhara katika Kijiji cha Msange Wilaya ya Singida vijijini.

"Mheshimiwa Samia akishamaliza kutangaza Ilani ya uchaguzi na sera za CCM, ataondoka kuelekea jimbo la Singida Magharibi katika Kijiji cha Puma kilichoko Tarafa ya Ihanja na baada ya hapo ataelekea Singida mjini kwa mapumziko", alisema.

Kaburu alisema kesho kutwa Mama Samia na msafara wake wataelekea Kijiji cha Iguguno jimbo la Iramba Mashariki Wilaya ya Mkalama NA akiwa hapo atafanya mkutano wa hadhara na kisha ataelekea Jimbo la Iramba Magharibi.

Alisema baada ya kumaliza mikutano yake ya kampeni katika maeneo hayo ataondoka kuelekea mkoani Tabora kuendelea na kampeni.

 Kaburu, ametumia nafasi hiyo kuwaalika wana CCM na wananchi wote kwa ujumla  mkoani hapa kuhudhuria mikutano hiyo ya hadhara.


Share To:

Post A Comment: