NA HERI SHAABAN
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu kuzindua Kampeni za Ubunge Wilayani Ilala Septemba 5.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisi za CCM Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi Wilaya Ilala Said Sidde alisema,uzinduzi wa Kampeni za ubunge Wilaya ya Ilala,zitazinduliwa Jimbo la Segerea siku ya Jumamosi viwanja vya Tabata Shule kuanzia saa mbili asubuhi ambapo mgeni rasmi Mgombea Mwenza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu.
"Kampeni zetu za ubunge na udiwani CCM wilaya ya Ilala tunazindua Jumamosi Septemba 5 mgeni rasmi mgombea Mwenza wa Jamhuri ya Muungano Mama Samia Suluhu nawaomba wana CCM wote tujitokeze kwa wingi viwanja vya TABATA shule shughuli yetu itaanza asubuhi saa mbili "alisema Sidde.
Aidha Sidde alesema kampeni hizo kwa Jimbo la Ukonga zitazinduliwa Septemba 6 Viwanja vya Kampala kuanzia saa mbili asubuhi .
Alisema Chama cha Mapinduzi CCM wilaya Ilala kinapeperusha bendera yake ya CCM kwa kuwanadi wagombea udiwani wa kata zote 36 na wabunge wa jimbo la Segerea Bonah Ladslaus,Ukonga Jerry Silaa na jimbo la Ilala Mussa Zungu.
Alisema chama hicho kimejipanga vizuri kitashinda majimbo yake yote ya uchaguzi wilaya ya Ilala
Mwisho
Post A Comment: