Na Said Mwishehe, Bahi
MGOMBEA Urais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.John Magufuli amemuomba dereva wake kumuombea kura za urais kwa wananchi wa Wilaya ya Bahi jijini Dodoma.
Wakati anazungumza na maelfu ya wananchi wa Wilaya ya Bahi ambao wamejitokeza kwenye Mkutano wa Kampeni za Chama hicho, Dk.Magufuli baada ya kuelezea kwa kina mafanikio ya maendeleo katika wilaya hiyo alimuita dereva wake ambaye anatoka jijini Dodoma amuombee kura
Baada ya kuitwa na Dk.Magufuli ,dereva wake alisimama mbele ya wananchi wa Wilaya ya Bahi waliokuwa wamejitokeza kwa wingi katika mkutano huo ambapo aliwaambia yeye anatokea Wilaya ya Kongwa, hivyo anamuombea kura tena ziwe za kutosha aweze kuendelea kuwaletea maendeleo.
Hata hivyo dereva huyo wakati anaomba kura alikuwa akiomba kwa lugha ya kabila la Wagogo ambapo wananchi nao walimjibu kwamba mgombea huyo atapata kura nyingi maana ambayo ameyafanya katika Awamu ya miaka mitano wameona maendeleo makubwa yaliyofanyika na wanamini akipewa tena miaka mingine mitano atafafanya makubwa zaidi .
Wakati akiomba kura hizo wananchi walionekana wakiwa wenye furaha na baada ya hapo Dk.Magufuli aliendeelea kueleze namna ambavyo CCM imejipanga kutekeleza miradi ya maendeleo na kwamba yaliyofanyika katika miaka mitano iliyopita ilikuwa ni onja onja tu na akipewa miaka mitano mingine atafanya kazi zaidi ya sasa.
Post A Comment: